Jumatatu, 13 Oktoba 2014

ELIMU KIDEDEA MPIRA WA MIGUU SHIMIWI



Wizara   ya Elimu na Mafunzo  ya  Ufundi imeendeleza ubabe katika mchezo wa mpira miguu  baada ya Timu yake ya Elimu  Sport kuibuka na ushindi wa kwanza na  kutwaa kombe ikiwa ni mara ya tatu mfululizo katika Mashindano ya 34 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2014 .
Katika Ushindi huo Elimu Sport ilipambana na Vilabu 60 vya  Wizara na Idara za Serikali mbalimbali, na kufanikiwa kufikia fainali anbapo ilishindana na timu ya Wizara ya Uchukuzi na kuwashinda kwa mabao 5 – 3 na kupelekea ushindi huo.
 Aidha, Elimu Sport  ilishiriki michezo mingine ambapo katika mchezo wa  kurusha  vishale   (Darts) iliibuka  mshindi wa  pili na kuibuka na   kikombe. Katika mchezo wa Riadha  Mita  mia  moja   kwa upande wa  wanaume  imepata  medali ya  Fedha baada ya kuibuka mshindi wa pili.
























Ijumaa, 10 Oktoba 2014

WAZIRI MKUU AKAGUA UTEKELEZAJI MRADI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU SUA



Waziri Mkuu, Mhe. Kayanza Peter Mizengo Pinda (MB) ametembelea na kukagua Mradi wa  Sayansi, Teknologia na Elimu ya Juu katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Mkoani Morogoro, na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo chuoni hapo.

Mhe, Waziri Mkuu amefanya ziara hiyo jana, ambapo alipata nafasi ya kujionea majengo matatu, vifaa vya kisasa vya kujifunzia na kufundishia katika maabara za chuo pamoja na kupata nafasi ya kuongea na wanajumuiya ya chuo wakiwemo waliopata ufadhili wa mafunzo kutoka katika mradi huo.

Mradi wa Sayansi, TeknoloJia na Elimu ya Juu katika  chuo Kikuu cha Sokoine umejenga jengo la ghorofa mbili kwa ajili ya idara ya Uchumi kilimo na biashara, jengo la ghorofa moja katika idara ya uandisi kilimo na Mipango Ardhi. Pia imejenga maabara ya kisasa ya Zoolojia. 

Aidha, mradi umewezesha kuanzishwa kwa mitaala mipya miwili ya Shahada ya Uzamili katika uhakiki wa ubora na Usalama wa Chakula na Mtaala mwingine ni ule wa Uhandisi na Usimamizi wa Uchakataji mazao baada ya kuvunwa.

Makamu Mkuu wa Chuo Bw Gerald Monella, alisema mradi huo umesaidi kupatika kwa ofisi za wahadhiri na wafanyakazi wengine wa Chuo, kufadhili wahadhiri 21 katika mafunzo Uzamili na Uzamivu, ujenzi wa miundombinu ya madarasa na maabara pamoja na ununuzi wa vifaa vya maabara na TEHAMA.






Jumatano, 8 Oktoba 2014

WAZIRI MKUU KUKAGUA MRADI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU



 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda atatembelea na kukagua Mradi wa Mradi wa STHEP (Science Technology and Higher Education Project); unaotekelezwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, kuanzia tarehe 9 – 11 Oktoba.

Waziri Mkuu atatembelea Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) kilichopo Mkoani Morogoro, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo kishiriki cha Elimu Chang’ombe.  Pamoja na mambo mengine Waziri Mkuu atakagua vifaa vilivyo nunuliwa na mradi, Majengo yaliyojengwa na ukarabatiwa. 

Tokea 2009 Mradi wa STHEP umedahili na kuwasomesha (enrolled)  jumla ya wakufunzi na watumishi 188 wa taasisi za umma masomo ya shahada ya uzamivu (PHD), na jumla ya watumishi 208 masomo ya uzamili (Masters) katika fani za sayansi tekinoljia na ualimu. Hawa wamedahiliwa katika vyuo bora huko dunia ya kwanza (Uingereza nk aslilimia 30%) Dunia ya pili (South Africa na kwingineko (asilimia 30%) na waliobaki hapa nchini (40%).
Jumla ya watumishi wa taasisi za Elimu 188walidahiliwa katika  shahada ya uzamivu (PhD) kati yao wanawake wakiwa ni 57 (30%). Na pia kati ya wadahiliwa 208wa masomo ya Uzamili (masters)ambapo wanawake walikuwa 44 (21%).

Hadi Julai 2014 jumla ya watumishi 210kamaasilimia 60% ya wote waliodahiliwa walikuwawamekamilisha masomo yao, na wameanza kutumikia taifa kwenye ufundishaji.
Kwa sasa mhitimu mmoja wa ngazi ya Uzamivu ana uwezo wa kufundisha karibu wanafunzi 100 wa Shahada ya Kwanza katika semesta moja na Wanafunzi 30 ngazi ya Uzamili. Aidha, utegemezi katika kuwatumia wahadhiri wa muda umepungua na hivyo kupunguza gharama.  Kwa mfano, katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, katika mwaka 2011/2012 idadi ya Wahadhiri wa muda ilipungua kutoka 98 hadi 57 na hivyo kupunguza gharama kutoka 237,495,550.00 hadi 138,135,167.00.

Aidha mradi wa STHEP umesomesha jumal ya watumishi 465 katika kozi za kitaalamu za muda mfupi (professional short courses).

(B2) Kujenga, kupanua na kukarabati vyumba vya mihadhara,  maktaba, maabara, karakana na miundo mbinu ya utafiti (Civil Works)
Jumla ya majengo mbalimbali ya mihadhara, maktaba, ofisi, mitambo ya kufundishia mipya 25 imeshajengwa katika vyuo vikuu mbalimbali nakati ya hayo 14 yamenza kutumika na 11 hayajaanza kutumika yakisubiri fenicha, kuunganishwa mifumo ya umeme maji taka na marekebisho mengine. 

Majengo haya yatatumiwa na jumla ya wanafunzi wa elimu ya juu 47,622nchini kote kujifunzia. Pia STHEP katika majengo haya inawapatia ofisi wahadhiri, wakufunzi, wakutubi,wataalamu wa maabara na wengine 1794katika taasisi 8 ARU, DUCE, DIT, OUT, MUCE, SUA,  and UDSM. Pia jumla ya wananchi 2,194 wanaozunguka vyuo (society) watanufaika na miundo mbinu za kitafiti zilizojengwa (mfano mitambo ya kusafisha taka ya STHEP chuo cha ARU) 

(B3) Vifaa vya kufundishia vikiwemo magari, vifaa vya maabara na tehama, vitabu nk (Procurement of lab, ICT equipments) 

B3.1 Vifaa vya tehama zikiwemo tarakilishi (PCs) nakompyuta mpakato (laptops) na vifaa vingene vya Tehama 1,831 vitakavyotumika kufundishia wanafunzi 5400 kila wiki
B3.2: Vifaa vya maabara za sayansi  5634 vitakavyotumiwa kila wiki na jumla ya wanafunzi 16,600
 B3.3: Vitabu: Jumla ya Vitabu vya kiada kwa sayansi, tekinolojia na ualimu vipatavyo 6,121. 
 
B3.4: Magari: Jumla ya magari 19 yamenunuliwa na STHEP.
Magari yaliyonunuiwa ni ya aina mbalimbali yakiwemo mabasi madogo (minibuses) pamoja magari ya 4x4 (Off Road kama Land Cruiser Hardtops) kwa ajili ya safari za masomo na utafiti. Kila wiki magari haya 19 yatatumiwa na wanafunzi na waalimu 133

(B4)KUJENGA UWEZO WA TAASISI ZAA KITAIFA ZA ELIMU

B4.1 STHEP KUJENGA UWEZO TUME YA VYUO VIKUU NCHINI

Mfumo wa Kielekroniki wa Udahili wa pamoja (Central Admission System)

Kupitia mradi huu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania imeweza kupata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutengeneza mfumo wa udahili wa Kielekroniki wa wanafunzi wanaojiunga Vyuo Vikuu hapa nchini, ambapo mwaka 2009/2010  jumla ya wanafunzi 40,479 walidahiliwa ikiwa ni wanaume 25,861 na wanawake 14,618 bila kutumia mfumo wa kielektroniki. 2010/2011 mfumo ulianza kutumika ambapo idadi ya udahili iliongezeka na kufikia 53,319; wanawake 19,824 na wanaume 33,495. Katika mwaka wa masomo 2012/2013 na 2013/2014 idadi ilizidi kuongezeka kutoka 44,715 hadi kufikia 52,537 ambapo idadi ya wanawake iliongezeka japo kwa kiasi kidogo kutoka 15,388 mwaka 2012/2013 hadi 18,858 mwaka wa masomo 2013/2014.

Mradi pia umewezesha Tume kubaini uwezo wa vyuo vilivyopo vya kudahili wanafunzi na kuweka bayana vigezo vya kujiunga na Vyuo Vikuu kwa kila programu ya masomo pamoja na kuokoa gharama ya nauli ikiwa ni kero kubwa kwa familia nyingi za Kitanzania. Mfano, kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa udahili wa Kielektroniki mwanafunzi alikuwa anatumia jumla ya shilingi 1,063,000/= kama gharama za nauli, malazi, chakula, ada ya maombi na gharama za mtandao kwa kuomba vyuo tofauti visivyozidi 7. Baada ya kuanza kutumika kwa mfumo huo mwanafunzi anaweza kukamilisha maombi yake kwa kiasi cha shilingi 80,000/=tu, hivyo kuokoa kiasi cha shilingi 983,000/=.

Mfumo wa kielektroniki umeweza pia kubaini waombaji wenye mahitaji maalum kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii na hivyo kuwadahili kwenye Vyuo Vikuu vinavyokidhi mahitaji yao. Kwa mfano; katika udahili wa mwaka 2013/2014, Tume iliweza kubaini jumla waombaji 394 wenye mahitaji maalum. Kati ya hao, wanawake walikuwa 165 na wanaume 229.

Mfumo huu vilevile umeweza kuondoa tatizo la matumizi ya vyeti vya kughushi wakati wa kuomba udahili kwa kuwa hivi sasa kinachohitajika ni namba ya mtihani tu. Matokeo yanapatikana kwa mtandao kutoka katika mitandao ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

B4.2STHEP KUJENGA UWEZO BODI YA MIKOPO NCHINI

Utekelezaji waSTHEP ulijikita katika kuboresha mambo mawili
(i)                   Kuboresha mchakato wa uombaji mikopo
(ii)                  Kuboresha mfumo wa ufuatiliaji madeni

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ulianza katika mwaka wa fedha 2008/2009.

Mfumo mpya wa uombaji mikopo kwa tehama

Kupitia mradi huu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imeanzisha Mfumo wa tehama wa kuomba mikopo kupitia kwenye mtandao (Online Loan Application System) ambao ulianza kazi hapo Mei 2013 ambapo kwa mara ya kwanza jumla ya wanafunzi 115,322 waliomba mkopo kupitia mfumo wa Kielektroniki wakiwa sehemu/mikoa bila ya kufika ofisi za Bodi ya mikopo Dares Saaam kama ilivyokuwa hapo awali .
Aidha, viambatishi vyote vilitumwa kwa njia ya Tehama (EMS) ambapo wanafunzi hawakutakiwa kufika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Mfumo wa urejeshaji wa mikopo

Kiwango cha ufuatiliaji na urejeshaji wa mikopo kimeboreshwa kupitia miundo mbinu mbali mbali (software and databases)  pamoja na mafunzo kwa watumishi wahusika. Kutokana na maboresho hayo, marejesho ya mikopo yameongeza   kutoka kwa wadaiwa 41,321 sawa na asilimia 30 waliorejesha mikopo yao mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 39 sawa na wadaiwa 55,342  waliorejesha mikopo mwaka 2013.

C. CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI 

Mapungufu ya jumla ya US$ 7.5 milioni toka kwenye tengeo zima la bajeti ya mradi wa STHEP (Toka US$ 100 millioni hadi US$ 92.5 milioni). Makubalioano kati ya Benki ya Dunia na serikali yalifikiwa mnamo mwaka 2008 ambapo thamani ya Dola ya Marekani ilikuwa imeshuka sana kutokana na kudorora uchumi wa Dunia. Hivyo kiasi cha sarafu ya benki ya dunia SDR 60,800 zilizokuwa na thamani ya US$ 100milioni mwaka 2008 ilibadilika. Mwaka wa mwisho ya mradi  SDR 60,800 zilikuwa na thamani ya US$ 92.5 milioni tu na ndio zilizopatikana na kutuiwa na STHEP.
Hivyo taasisi zilikumbwa na mapungufu hayo ya Exchange loss na kukosa fedha za kukamilisha majengo na nk