Jumanne, 29 Machi 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi atembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akisikiliza  maelezo kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila kutoka kwa wasimamizi wa ujenzi


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akikagua maeneo  mbalimbali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila


 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akikaangalia ramani ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila kinachoendelea kujengwa.


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akizungumza na viongozi wa Chuo Kikuu  cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili pamoja na Wakandarasi (Hawapo Pichani)  kuhusu  ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila alipotembelea ili kuonea maendeleo ya ujenzi huo.


 
Moja ya Jengo la  Chuo Kikuu  cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila linaloendelea kujengwa

 



Alhamisi, 24 Machi 2016

Serikali yatoa zawadi kwa Halmashauri zilizotekeleza mipango ya kuboresha Elimu


Serikali kwa kushirikiana na wafadhili wa maendeleo wanatekeleza programu inayojulikana kama Lipa Kulingana na Matokeo ambayo inalenga kutoa zawadi kwa Serikali kuu na Halmashauri kulingana na utekelezaji ambapo kwa kuanzia vigezo vifuatavyo vimewekwa kwa ajili ya kupima utendaji wa Halmashauri. Vigezo vilivyowekwa viliangalia Eneo la Ruzuku zinazopelekwa shuleni.  Katika eneo hili Halmashauri 167 zilipimwa kwa kanuni ya kuchukua fedha iliyopelekwa shuleni.

Eneo lingine lililoangaliwa ni upatikanaji wa  Takwimu. Eneo hili liliangalia idadi ya shule zilizopo kwenye Halmashauri ambazo takwimu zake zimekusanywa na kuwekwa mtandaoni.  

Aidha, eneo lingine lililoangaliwa ni Uwiano wa Mwalimu kwa Mwanafunzi: Halmashauri zilipimwa kwa idadi ya shule ambazo zilikuwa na walimu wachache na zimeongezewa walimu. Hii ni kwa sababu Halmashauri zinapimwa uwezo wake wa kupunguza walimu kwenye shule zenye walimu wengi kupeleka kwenye shule zenye walimu wachache na pia kupanga walimu wapya kwenye shule zenye uhaba wa walimu.

 Jumla ya Kila Halmashauri ilitakiwa ipate dola za kimarekani 7,000. Katika hili Serikali kuu pia inapimwa katika uwezo wake wa kupeleka walimu kwenye Halmashauri na kwa tawkimu zilizokusanywa mwaka 2014 wakati wa kusambaza walimu. Halmashauri 112 zilikuwa na uwiano wa kati ya 1:35 -1:50, Halmashauri 25 zilikuwa na uwiano zaidi ya 1:50 na Halmashauri 27 zilikuwa na uwiano wa chini ya 1:35.


Halmashauri ya zilizofanya vizuri na kupata zawadi ni Mbinga iliyopata shilingi 331,234,275.00, Chato 302,637,899.56, Busega 282,677,815.00, Lushoto 267,403,689.33 Nkasi 262,991,890.00, Liwale 260,836,890.00,  Sikonge 244,679,555.61,  Mbarali 216,749,648.88, Mpanda 213,341,853.60 na Tabora 185,191,379.60