Jumanne, 24 Mei 2016




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


TAARIFA KWA UMMA
USAJILI WA SHULE ZA AWALI, MSINGI, SEKONDARI NA VITUO VINAVYOTOA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI NA SEKONDARI HURIA  

Serikali kupitia Sheria ya Elimu Sura ya 353 inaelekeza  shule zote kusajiliwa kabla ya kusajili wanafunzi. Azma hii ya serikali ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na utaratibu madhubuti wa kusimamia Ubora wa Elimu.

Hata hivyo, kumekuwepo na baadhi ya wadau wanaanzisha na kuendesha shule au vituo vinavyotoa elimu nje ya mfumo rasmi  bila kupata Usajili.

Wanafunzi wanaotoka katika shule au vituo hivi hufanya mitihani ya taifa ikiwemo  mtihani wa maarifa (QT)  na mitihani mingine ya Taifa (Kidato cha Nne na Sita)  kama watahiniwa wa kujitegemea. Aidha, baadhi ya wanafunzi hawa huingizwa kwa utaratibu usio rasmi kufanya mitihani ya Darasa la Nne na Darasa la Saba katika shule zilizosajiliwa pasipo kuzingatia mazingira ya mahali waliposomea hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kushindwa katika mitihani hiyo.

Kwa tangazo hili serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawataka wamiliki wote wa shule ambazo hazijasajiliwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi za Uthibiti Ubora wa shule Kanda, Wilaya au Idara ya Ithibati ya shule (Usajili) Makao Makuu ya wizara kabla au ifikapo tarehe 30/07/2016. Shule ambazo hazijafikia vigezo vya kusajiliwa, zitafungwa na hazitasajiliwa na Mwenye Shule husika atapaswa kuhamisha wanafunzi waliopo kwa gharama zake. 

Imetolewa na

Dkt. Leonard D. Akwilapo
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Maoni 2 :

  1. Nina maoni yangu juu ya elimu yetu ya Tanzania na ningeomba hayo maoni angalau yangeweza kuchapishwa humu na kumfikia waziri wa elimu. Nikubaliwa nitashukuru sana!
    Ni mimi mdau wa elimu

    alcherwega@ymail.com
    0758149715

    JibuFuta
  2. shikamooni wakubwa mm ni mwanafunzi wa chuo hapa tanzania kutucheleweshea pesa za field kisa uchunguz ni kitu kizuri ila kumbukeni chuo hakita simamisha ratiba yake na kukosa field ni direct disco.nawashauri tafuteni solution ya nataka kama waagiza watu kutoka wizarani kusimamia zoez la usahishaji wa pesa na kuwabana loan officers wa vyuo...au semeni kusain field ni kwa wanafunzi walio fanya ue tuu....hivo wasio wanafunzi hawato saini....chuo kinafunga ijumaa watu inabid waondoke kwaiyo u chunguzi unaweza kuisha alaf watu wakashindwa kuja kusain...naombeni mfanyie kaz hili mapema iwezekanavyo

    JibuFuta