Ijumaa, 7 Oktoba 2016

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA PROFESA JOYCE NDALICHAKO AWAFUKUZA WALIMU 4 WALIOSHIRIKI KUMPIGA MWANAFUNZI MBEYA. 





Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa JOYCE NDALICHAKO ametangaza kuwafukuza chuo walimu wanafunzi walioshiriki kitendo cha kumpiga mwanafunzi wa kidato cha TATU katika shule ya kutwa ya Sekondari mkoani MBEYA.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini DSM waziri NDALICHAKO amesema kuwa kitendo hicho ni cha kikatili, jinai na kuwa walimu hao wanafunzi hawafai kuendelea na taaluma hiyo ya ualimu na kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa.

Waziri NDALICHAKO amesema kuwa kwa mujibu wa taratibu za vyuo vikuu kitendo kilichofanyika ni kosa la jinai na kuwa hakiwezi kufumbiwa macho.


Waziri pia ametoa onyo kali kwa wanafunzi wanaokwenda kwenye mazoezi kwa vitendo  na kuwa kwenda kinyume na taaluma, mwanafunzi wa vitendo  anakuwa amepoteza sifa hivyo amewataka  kuzingatia maadili  ya  fani na  taaluma  wanazozisomea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni