Alhamisi, 1 Desemba 2016

China yakabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia


Serikali ya China imekabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuwezesha wizara kufanya kazi kwa weledi. vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu Prf. Saimon Msanjila ofisini kwake na Liu Yun

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Liu Yun alimwelezea Naibu Katibu Mkuu kuwa wanajisikia faraja kubwa kukabidhi vifaa hivyo kwa wizara kwani China na Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa karibu sana katika sekta ya elimu hasa katika upande wa elimu ya juu.

Vitendea kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na Dell desk compture 6, mashine ya kudurufu moja, scanner moja, video camera moja na komputa mpatako 10 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano

Ushirikiana huo umewezesha serikali hizi mbili kuweza kubadilishana wanafunzi wa elimu ya juu katika fani mbali mbali. Pia alimuelezea uanzishwaji wa mafunzo ya lugha ya kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam ambapo alisema hii ni ishara tosha ya ushirikiano uliotukuka.

Naye Naibu Katibu Mkuu alimshukuru Yun kwa msaada huo wa vitendea kazi ambapo alimuahidi kuwa vitafanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba inaongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi wanaofika ofisi hapo kupata huduma mbalimbali za kielimu.

Baadhi ya vtendea kazi vilivyotolewa na serikali ya China kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuboresha na kurahisisha utendaji kazi wa watumishi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi 


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakisoma na kujadiliana nyaraka mbalimbali za vifaa wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakiweka saini makubaliano ya kupokea vifaa vilivyotolewa na China wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni