Jumatano, 31 Agosti 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Ndalichako afunga Mafunzo ya Vijana kwa Mujibu wa sheria Ruvu JKT

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa JKT Ruvu  alipohudhuria sherehe za kufunga mafunzo ya vijana wa mujibu wa sharia Operesheni Magufuli zilizofanyika Ruvu JKT Mlandizi

 Mkurugenzi wa ElimuMsingi Nicholaus Burreta kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa JKT Ruvu  alipohudhuria sherehe za kufunga mafunzo ya vijana wa mujibu wa sharia Operesheni Magufuli zilizofanyika Ruvu JKT Mlandizi


 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiangalia mazoezi yanayofanywa na vijana (hawapo pichani) waliohitimu mafunzo alipohudhuria sherehe za kufunga mafunzo ya vijana wa mujibu wa sharia Operesheni Magufuli zilizofanyika Ruvu JKT Mlandizi

Baadhi ya vijana wa JKT waliokuwa katika mafunzo kwa mujibu wa sharia wakimuonyesha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia mazoezi ambayo wamejifunza kwa kipindi chote cha mafunzo yao katika Kambi ya Ruvu JKT



                                     
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akipokea salam kutoka kwa vijana waliohudhuria mafunzo kwa mujibu wa sharia wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo katika kambi ya JKT Ruvu


 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake kutoka kwa vijana waliohudhuria mafunzo kwa mujibu wa sharia wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo katika kambi ya JKT Ruvu
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika sherehe ya kufunga mafunzo ya vijana wa mujibu wa sharia operation Magufuli zilizofanyika katika kambi ya JKT Ruvu

Jumatano, 24 Agosti 2016


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


TAARIFA KWA UMMA



Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WEST), kwa mujibu wa Waraka Namba 4 wa mwaka 2014, imeipa Taasisi ya Elimu Tanzania mamlaka ya kufanya  uthibiti wa ubora wa vitabu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Itakumbukwa kuwa kabla ya mwaka 2014, ithibati kwa vitabu na vifaa vya kielimu ilikuwa inatolewa na Kamati ya Ithibati ya Vitabu na Vifaa vya Kielimu (EMAC), ambayo ilivunjwa mwaka 2013.


Kwa muktadha huo, Wizara inawaagiza wachapishaji wote wa vitabu vya Darasa la Nne hadi Darasa la Saba ambavyo vina ithibati ya EMAC kuviwasilisha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kufanyiwa tathmini. Ili kufanikisha zoezi hili nakala nne (4) za kila chapisho ziwasilishwe kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania kabla ya tarehe 30 septemba, 2016. Baada ya muda huo kupita, vitabu vyote ambavyo havitakuwa vimewasilishwa na kuhakikiwa na Taasisi hiyo vitafutwa katika orodha ya vitabu vyenye ithibati.

Baada ya zoezi la uhakiki kukamilika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI, itafanya ufuatiliaji kwenye shule na maduka ya vitabu ili kuhakiki utekelezaji wa agizo hili.

Aidha, hatua stahiki zitachukuliwa kwa wauzaji/wachapishaji watakaoendelea kuuza vitabu vitakavyokuwa vimefutwa.



Imetolewa na:



Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akabidhi Chuo cha Ualimu Kitangali kwa Wakandarasi


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akiingia katika Chuo cha Ualimu Kitangali alipokwenda kukabidhi Chuo hicho kwa wakandarasi wa ujenzi kwa ajili ya kufanya ujenzi majengo mapya ya chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akipata maelezo kutoka kwa mkandarasi (hayupo pichani) juu ya ujenzi wa  Chuo cha Ualimu Kitangali alipokwenda kukabidhi Chuo hicho kwa wakandarasi wa ujenzi kwa ajili ya kufanya ujenzi majengo mapya ya chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni chuoni hapo.



Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akifanya ukaguzi kwenye ya jiko linatumika kwa jili ya kupikia chakula cha wanafunzi alipokwenda kukabidhi Chuo hicho kwa wakandarasi wa ujenzi kwa ajili ya kufanya ujenzi majengo mapya ya chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akikabidhi mkataba pamoja na michoro kwa mmoja wa wakandarasi watakaofanya kazi ya ujenzi ya miundombinu ya Chuo cha Ualimu Kitangali alipokwenda kukabidhi Chuo hicho kwa wakandarasi wa ujenzi kwa ajili ya kufanya ujenzi majengo mapya ya chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni chuoni hapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akikabidhi mkataba pamoja na michoro kwa mmoja wa wakandarasi watakaofanya kazi ya ujenzi ya miundombinu ya Chuo cha Ualimu Kitangali alipokwenda kukabidhi Chuo hicho kwa wakandarasi wa ujenzi kwa ajili ya kufanya ujenzi majengo mapya ya chuo hicho. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni chuoni hapo.


Jumanne, 23 Agosti 2016

Serikali yawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma Kuandika na Kuhesabu


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiongea na Wawakilishi kutoka kamati ya Global Partnership for Education  wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji ya  Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara 



 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiongea na Wawakilishi kutoka kamati ya Global Partnership for Education  wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji ya  Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara



Kaimu  Mkurugenzi wa Sera na Mipango  wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Gerald Mweli akiongea na Wawakilishi kutoka kamati ya Global Partnership for Education  wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji ya  Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara




 Baadhi ya wajumbe wa kikao wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na wasimamizi wa Mradi huo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji ya  Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara


Baadhi ya wajumbe wa kikao wakifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na wasimamizi wa Mradi huo wakati wa kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji ya  Mradi wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara

Ijumaa, 19 Agosti 2016

Mamlaka ya VETA yaagizwa kufanya tathmini ya mafunzo wanayotoa


Waziri wa elimu, Sayansi naTeknolojia Mhe. Profesa, Joyce Ndalichako ametoa mwezi mmoja kwa mamlaka ya VETA kufanya tathmini ya mafunzo wanayotoa katika vyuo vyote nchini ili kuona kama yanakwenda sambamba na matakwa ya serikali ya kuwa na wataalamu watakaokwenda kufanya kazi katika viwanda.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo alipofanya ziara leo katika Chuo cha VETA Kipawa ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake ambazo amekuwa akizifanya katika vyuo hivi ili kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao.

Alisema katika vyuo ambavyo ametembelea amekutana na changamoto za kuwepo kwa mashine ambazo zimeachwa bila kufanyiwa ukarabati na kuwa na kutu na nyingine ni nzima lakini hazitumiki wakati vipo vyuo ambavyo havina vitendea kazi hivyo

“Ni vizuri kukawepo na usawa wa mahitaji katika vyuo vyote vya VETA kila mkoa kulingana na uhitaji na sio vyuo vingine vinakuwa na vifaa na vingine havina au vilivyopo kutotosheleza mahitaji.“ Alisema Ndalichako.

Katika hatua nyingine Profesa Ndalichako ameitaka Menejimenti ya VETA kuweka mifumo yao ya mapato vizuri ili fedha zinazopatikana kutokana na kazi wanazozifanya ziweze kuendeleza mafunzo yatolewayo katika vyuo hivyo.

Aidha, amewataka pia kuhakikisha udahili wa wanafunzi unaofanyika unaendana na ukubwa wa vyuo ili kutimiza azma ya Serikali kuwa na vijana wengi wanaopata ajira sio tu ya kuajiriwa lakini pia waweze kuajiri wengine.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Bw. Geophrey Sabuni amesema Chuo cha VETA Kipawa kinatoa mafunzo katika masuala ya Tehama, mafunzo ambayo yanalenga katika kuhudumia viwanda katika teknolojia ya juu zaidi.

Alisema matokeo ya mafunzo wanayotoa yanajidhihirisha pale wanafunzi wao wanapokwenda mafunzo kwa vitendo kwani wengi wao wanapata ajira na kushindwa kurudi chuoni hapo kumalizia mafunzo yao.


Chuo cha VETA Kipawa kinatoa mafunzo ya TEHAMA na kutoa Tuzo kuanzia ngazi ya 1 hadi 3 pamoja na stashahada ya TEHAMA.










Jumanne, 16 Agosti 2016

Wizara za Elimu Zanzibar na Tanzania Bara kuendeleza Ushirikiano

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Mhe.Prof. Joyce Ndalichako mwishoni mwa wiki amekutana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma  ambapo walizungumzia masuala mbalimbali yahusuyo Sekta ya Elimu ikiwemo kuendeleza  ushirikiano wa masuala ya Elimu ambao umekuwepo tangu awali.

Mhe. Riziki alisema anatamani kuona walimu kutoka Zanzibar wanapata nafasi ya kukutana na walimu wenzao kutoka bara ili waweze kubadilishana na kupeana uzoefu wa  mbinu mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi ili kuweza kuboresha elimu itolewayo.

 ‘Kuna maeneo tofautitofauti katika kufundisha yanahitaji kutumia mbinu mbalimbali ili wanafunzi wetu waweze kuelewa, si vibaya walimu hawa wakakutana na kubadilisha uzoefu wa namna ya kufundisha katika maeneo hayo’ alisema Mhe. Riziki

Akizungumza katika kikao hicho cha kuimarisha mahusiano, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Ndalichako alisema ni vizuri kuendeleza misingi ya Ushirikiano katika masuala ya elimu ili kudumisha Muungano wetu. Alisema Wizara ya elimu ni kubwa na inafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi zake ambazo zina mamlaka kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo kulingana na maeneo wanayoyasimamia.

Ili kwenda sambamba na kudumisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania Bara na Zanzibar  Waziri Ndalichako alizitaka taasisi  za elimu zinazoshughulika na Masuala ya Muungano kutoa taarifa kwa wakati ili kutochelewesha utekelezaji wa masuala ya elimu kwa upande wa Zanzibar na kuleta changamoto zisizokuwa za lazima hapo baadae.

Aidha Katika kuendeleza ushirikiano kwa upande wa walimu kupeana uzoefu, Prof Ndalichako aliliagiza Baraza la Mitihani la Tanzania kwa kuanzia lipitie script za matokeo ya kidato cha sita kwa upande wa Zanzibar  ili kuona maeneo ambayo wanafunzi wameshindwa zaidi ili kuweza kundaa utaratibu wa kuwakutanisha walimu wanaofundisha masomo hayo waweze kupeana uzoefu kwa lengo la kuboresha.


Naye Naibu Waziri wa elimu Mhe. Mhandisi . Stellah Manyanya alisema ni vizuri Wizara ikaratibu utaratibu wa watendaji wa masuala ya kielimu kutoka Bara kukutana na wale wa Zanzibar ili kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoleta chanagamoto katika utekelezaji wa masuala ya kielimu kwa lengo la kuboresha.