Alhamisi, 15 Machi 2018

Maafisa Habari wa Serikali watoa msaada kwa Shule ya Laibon


Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali Leo wamekabidhi msaada wa Vitabu, Madaftari, kalamu na Matanki mawili ya kuhifadhia maji katika Shule ya Msingi Laibon iliyopo mkoani ARUSHA.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa hao- TAGCO, Pascal Shelutete amesema lengo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali za kutoa Elimu bure.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rashid Njarita ameshukuru kupokea msaada huo ambapo amesema matanki ya maji yataondoa changamoto ya maji iliyokuwepo shuleni hapo.

Msaada uliotolewa unathamani ya shilingi milioni mbili na laki tano.

Mwenyekiti wa Chama Cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali - TAGCO, Pascal Shelutete akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Laibon Rashid Njarita Madaftari kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.
Maafisa hao wa Mawasiliano wanashiriki kikao kazi ambacho kinalenga kujengeana uwezo wa namna bora ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.


Kikao hicho kimeanza Machi 12 na kitamaliza Machi 16, 2018 huku kauli mbiu ya mkutano huo inasema Je? Mawasiliano ya kimkakati yanachagiza Vipi Tanzania ya Viwanda.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abass akimkabidhi daftari mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Laibon iliyopo mkoani Arusha.Hakuna maoni:

Chapisha Maoni