Alhamisi, 15 Novemba 2018

DKT. AKWILAPO AZITAKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU KUFANYA TAFITI ZA KITAALAMU


Serikali imezitaka Taasisi za Elimu ya Juu nchini kutimiza wajibu wake wa kufanya tafiti za kitaalamu kwa kushirikiana na wadau ili kuongeza ufahamu kwa jamii na kuisaidia serikali kwenye kutunga na kusimamia sera utungaji na usimamizi wa sera mbalimbali za nchi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Katibu MkuuWizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka waWadau wa Tafiti kwa Maendeleo shirikishi uliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amezitaka Taasisi zinazohusiana na Tafiti kutafuta namna ya kufikisha matokeo ya tafiti hizo kwenye jamii kwa lengo la kuwaletea wananchi Mabadiliko na Maendeleo.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza na wadau waElimu kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa mwaka wa wadau wa tafiti kwa maendeleo shirikishi uliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo amezita kataasisi za elimu ya juu kufanya tafiti ili kuisaidia serikali  kutunga sera.



“Hakuna asiyefahamu kuwa Elimu ni chombo muhimu kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii, na kuwakupitia Elimu ndiyo njia pekee inayoweza kutoawataalamu wenye ujuzi wa kusaidia jamii kwenye kilanyanja, hivyo ni wakati muafaka kwa Taasisi za Elimu kulitambua hilo na kujua nyakati za sasa zinahitaji pia ufahamu wa masuala ya kidijitali,”alisistiza Dkt. Akwilapo.

Kwa upande wake Balozi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg, amesema Shirika la Maendeleo la Kimatiafa (SIDA) litaendelea kuisaidia Tanzania kujikwamua kiuchumi hususani kwenye viwanda kupitiakazi za kitaaluma kupitia Shirika hilo.

Akizungumza katika mkutano huo wa mwaka wa Wadau wa Tafiti kwa Maendeleo shirikishi Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Cuthbert Kimambo amesema ni dhahiri kuwa nchi ya Sweden imekuwa na mshusiano na ushirikiano mzuri na Tanzania katika sekta ya Elimu, na kupitiamradi huo unaojumuisha UDSM, ni hatua nzuri yakuisaidia serikali na wananchi kwa ujumla kufanyashughuli zao kitaalamu na kufikia Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akiangalia na kupata maelezo kuhusu ufugaji wa samaki mara baada ya kufungua mkutono wa Kwanza wa mwaka wa wadau wa tafiti kwa maendeleo shirikishi uliofanyika jijini Dar esSalaam.

Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) unawashirikishawatunga sera, wadau kutoka sekta ya umma na binafsi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni