Jumanne, 27 Novemba 2018

RAIS MAGUFULI AZINDUA MAKTBA YA KISASA KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI.

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli leo amezindua Maktaba ya kisasa kwa ukanda wa Afrika Mashariki iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) iliyojengwa kwa thamani ya dola milioni 41 Sawa na fedha za Kitanzania shilingi bilioni 90.

Akizungumza jijini Dar es salam wakati wa hafla ya kuzindua Maktaba hiyo iliyojengwa kwa msaada wa Serikali ya China Rais Magufuli amempongeza mkandarasi alyojenga Maktaba hiyo kwa kukamilisha mradi kwa wakati na kwa kiwango Cha juu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli akizindua jengo la Maktaba ya kisasa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako na balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke walishiriki uzinduzi huo.

Rais Magufuli pia ameishukuru serikali ya China kwa kuwa marafiki wa kweli kwa nchi ya Tanzania Kwa kutoa  msaada wa ujenzi wa maktaba hiyo pamoja na misaada mingine ya Maendeleo bila masharti yeyote.

“Tutaendelea kuenzi mahusiano mazuri yaliyoanzishwa na waasisi wa serikali hizi mbili ambazo ni Tanzania na China, na kuwa kuwepo kwa mahusiano kumekuwa na tija katika Kujiletea Maendeleo na kuwa misaada imekuwa ikitokewa bila masharti yoyote,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli katika hotuba yake amekitaka Chuo Kikuu kuendelea kusimamia maadili, heshima ya Chuo kikuu na kuhakikisha Elimu inayotolewa ni ya  viwango ili kulinda hadhi ya Chuo hicho.

Rais John Magufuli akikabidhiwa mfano wa ufunguo na balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke kwa ajili ya kufungulia maktaba ya kisasa ambayo amezindua leo katika Chuo kikuu cha Dar es salaam, jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli pia amewataka  wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na wale wa nje ya Chuo kuhakikisha wanaitunza maktaba hiyo ili idumu na iweze kutumiwa na vizazi vijavyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezitaka Taasisi za Elimu ya Juu kuacha kutumika kama vichaka vya kuvunja sheria na kufanya ubadhirifu wa fedha za Umma.

“Tunazitaka  Taasisi zote za Elimu ya Juu kuhakikisha zinakuwa ni  mfano wa kuigwa na siyo kuwa mstari wa mbele katika kushiriki vitendo vya ubadhirifu, na kuwa watumishi wa Taasisi hizo  ni watumishi wa Umma na kama walivyo watumishi wengine na kuwa yeyeote atakyekwenda kinyume Sheria itachukua Mkondo wake,” alisisitiza Waziri Ndalichako.
Viongozi waandamizi wa Serikali kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali wakifuatilia uzinduzi wa maktaba ya Kisasa ya UDSM jijini Dar es salaam, maktaba hiyo imejengwa kwa msaada wa Serikali ya china kwa gharama ya shilingi bilioni 90.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Prof. William Anangisye amesema Maktaba ni chombo muhimu katika kujiendeleza na kuwa maktaba hiyo ya kisasa itatumiwa na wafunzi pamoja na watafiti mbalimbali katika kujiongezea maarifa.

Rais John Magufuli akimshukuru balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Wang Ke kwa kufanikisha ujenzi wa maktaba ya kisasa iliyojengwa katika Chuo kikuu cha Dar es salaam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni