Alhamisi, 7 Februari 2019

DKT. AKWILAPO AZINDUA DIRISHA LA SOMO LA KIFARANSA KATIKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amezindua dirisha la taarifa za kimasomo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam litakalowapa fursa wanafunzi na wadau hasa wa somo la lugha ya kifaransa kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na fursa za masomo zinazopatikana nchini Ufaransa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akijadiliana jambo na Balozi wa Ufaransa Mhe. Frederic Clavier wakati wa hafla ya uzinduzi wa dirisha la taarifa za kimasomo katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam litakalowapa fursa wanafunzi na wadau hasa wa somo la lugha ya kifaransa kupata taarifa kuhusiana na fursa za masomo nchini Ufaransa.

Kituo hicho kitawawezesha wanafunzi na wadau wengine kuingia katika mfumo wa kompyuta na kupata taarifa hizo hasa za kimasomo, aina za kozi, na vyuo vilivyopo nchini humo kwa ajili ya kujiunga.

“Ufaransa wanataka kuwa moja ya mataifa yanayoongoza kwa kukaribisha wanafunzi wengi wa kigeni nchini mwao, kwa sasa wanashika nafasi ya nne ili kufikia lengo la kushika nafasi ya kwanza wameanzisha kampeni inaitwa STUDY in FRANCE ambapo ifikapo 2027 wanatarajia kuwa na idadi ya wanafunzi wa kigeni laki 5 wanaotoka katika nchi mbalimbali,” alisema Dkt. Akwilapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa dirisha la taarifa za fursa za kimasomo zinazopatikana nchini Ufaransa. Dirisha hilo limezinduliwa katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa nchi ya Ufaransa ina wafunzi wasiozidi elfu 25,000 hivyo kupitia dirisha hilo kutasaidia wadau kupata  taarifa kwa haraka zaidi  kupitia dirisha hilo la kuaminika.

Kwa maelezo zaidi kuhusu namna ya kujiunga na masomo nchini Ufaransa fika katika Ofisi zao zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akisalimiana na Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wawakilishai kutoka ubalozi wa Ufaransa wakati alipowasili chuo hapo kuzindua dirisha la taarifa za fursa za kimasomo zinazopatikana nchini Ufaransa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni