Jumanne, 6 Septemba 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr. John Pombe Maghufuli afanya ziara kukagua ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako akipata maelezo ya awali kutoka kwa Profesa Florens Luoga (Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma) kuhusu ujenzi wa mabweni ya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati alipotembelea eneo la mradi huu muda mfupi kabla ya Rais kuwasili.Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish.



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea Mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).





Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish akisalimiana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli wakati alipotembelea Mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
 


 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli  akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa TBA Aktecti (Arch) Elius A.. Mwakalinga kuhusu mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati alipotembelea Mradi huo chuoni hapo. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako.
 










Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli akikagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati alipotembelea Mradi huo. Kushoto ni Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako.





 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako akimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli  kwa uamuzi wa kujenga mabweni katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni hatua katika kuleta ubora wa elimu.


  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wanajumuiya ya Chuo Kikuu pamoja na Wafanyakazi wa Mradi huo mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa mabweni hayo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr.John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.