Jumatatu, 20 Februari 2017

Serikali za Tanzania na China zatia saini ujenzi wa Chuo cha VETA Kagera



 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi na Mwakilishi wa Masuala  ya Uchumi na Biashara ya Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong wametiliana saini makubaliano ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA kitakachojengwa  Gera mkoani kagera


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi akibadilishana hati za makubaliano (MOU) na Mwakilishi wa Masuala  ya Uchumi na Biashara wa Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong mara baada ya kutiliana saini.

Alhamisi, 16 Februari 2017

Mkutano wa SDGs4 unaendelea leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini DSM nchini Tanzania

Mawaziri kutoka nchi Kumi tatu, wawakilishi, mabalozi na wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri wa elimu katika mkutano wan chi za Ukanda wa Afrika Mashariki wa akuaanisha changamoto zinazofanana katika mfumo wa  elimu ili kubadilishana uzoefu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo. Mkutano huo unatarajiwa kuitimishwa leo jioni.







Mawaziri kutoka nchi Kumi tatu, wawakilishi, mabalozi na wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri wa elimu katika mkutano wan chi za Ukanda wa Afrika Mashariki wa akuaanisha changamoto zinazofanana katika mfumo wa  elimu ili kubadilishana uzoefu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo. Mkutano huo unatarajiwa kuitimishwa leo jioni.







MKUTANO WA NCHI 13 ZA UKANDA WA A. MASHARIKI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDFELEO ENDELEVU SDGs4 YA ELIMU 2030

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifungua mkutano wa nchi kumi na tatu za ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu utekelezaji wa Malengo yaMaendeo Endelevu SDGs4 ya elimu 2030 ambao unafanyika tarehe 15/02/2017 hadi tarehe 16/02/2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.





Waziri wa Elimu amebainisha malengo ya mkutano huo kuainisha changamoto zinazofanana na kubadilishana uzoefu wa namna wa kukabiliana na changamoto hizo, ambapo kwa pamoja wanahitaji  uwepo kwa elimu jumuishi yenye usawa bila kujali wanakotoka.





Jumatatu, 6 Februari 2017

Waziri wa Elimu atoa vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika sekta ya Elimu nchini.


    Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni Mia Saba na Nne, Mia Sita Ishirini na Saba Elfu na Mia Nane Hamsini Na Sita (704,627,856/=) kwa Halmashauri ya kwanza ya Kaliua Kati Ya Halmashauri zote Nchini zilizoshindanishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [ (P4r).




      Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi cheti cha ushindi kwa Halmashauri ya Kaliua iliyopata ushindi wa kwanza Kati ya Halmashauri zote Nchini zilizoshindanishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [ (P4r).


Jumanne, 6 Desemba 2016

Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakutana Dar


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Serikali ya Canada  na Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira  unaendesha warsha ya siku tatu inayojadili Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi  kwa kushirikisha mfumo shirikishi, mafunzo ya kuendeleza ujuzi, na Masuala ya Jinsia. 

Warsha hii inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii (Bustani) inalenga kusaidia uanzishwaji wa mfumo wa kuongeza  ushirikiano miongoni mwa watendaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi sekta nchini.

Wadau mbalimbali wameshirikishwa katik warsha hii ambayo imewaleta pamoja wadau wa elimu ya ufundi na wawakilishi mbalimbali wakubwa, mashirika mbalimbali yanayotoa elimu na mafunzo, watu binafsi, waajiri na vyama vya waajiri, soko la ajira mashirika ya habari na mashirika ya kiraia ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi ya kuwezesha wanafunzi wanaohitimu katika  Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi anakuwa na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa.

:   Mshauri Mwandamizi wa Ufundi na mwakilishi wa Vyuo na Taasisi  zinazosaidia vyuo na Vyuo vya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi Canada Dr. Alan Copeland  (aliyesimama) ambaye kwa sasa anasimamia Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira  nchini akizungumza katika warsha ya siku tatu ya wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi inayofanyika jijini Dar es Salaam inayojadia masuala mbalimbali kuhusu sekta hiyo.





Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu ya Ufundi na Mafunzo Ufundi Stadi. Warsha hii imewaleta pamoja wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi inavyoweza kufanya vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa wakiwa na ujuzi stahiki.

Waziri wa Elimu hakutana na Ujumbe wa Benki ya Dunia



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na wajumbe kutoka Benki ya Dunia waliofika wizarani kuongea naye masuala mbalimbali ya Elimu na jinsi ya benki hiyo itakavyoendelea kusaidia sekta ya elimu nchini wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Sajitha Bashir, Cornelia Jesse na Gayle Martin kutoka Benki ya Dunia.
Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Elimu aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya elimu ambayo imekuwa chachu ya kuleta maboresho katika sekta ya elimu nchini. Hivyo amewaomba kuendelea kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika elimu ili kuhakikisha inaendelea kuboreshwa na kuwapa fursa watoto waengi wa Kitanzania kupata elimu iliyo bora.
Naye Mjumbe kutoka Benki ya Dunia Sajitha Bashir amemuhakikishia Waziri wa Elimu kuwa Benki ya Dunia itaendelea kufadhili miradi ya Elimu nchini pale itakapoitajika. Aidha, alisisitiza kuwa miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ni lazima itoe matokeo yanayokusudiwa

Waziri wa Elimu azindua mashindano ya Ujuzi


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa Mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.