Jumatatu, 9 Septemba 2019

SERIKALI YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU VYUO VYA SERIKALI


Katibu Mkuu wa Wizara  ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza sehemu ya pili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu katika vyuo 35 vya serikali.

Akitoa taarifa hiyo jijini Dodoma mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo amesema jumla ya wanafunzi 2,834 wamechaguliwa kujiungana mafunzo ya ualimu ambapo kati yao 1,013 ni wa Astashahada na 1,821 ni wa Stashahada.

Dkt. Akwilapo ameongeza kuwa hadi sasa jumla ya wanafunzi 11,028 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vya serikali ambapo kati yao wanafunzi 8,194 walichaguliwa awali na TAMISEMI na 2,834 wamechaguliwa na NACTE.

Aidha, Dkt. Akwilapo amewataka wanafunzi hao waliochaguliwa kuripoti katika vyuo walivyopangiwa kuanzia tarehe 20 Septemba mwaka huu na kwamba mwisho wa kuripoti ni tarehe 6 Oktoba mwaka huu.  Amesisitiza wahakikishe wanaripoti ndani ya muda huo kwani baada ya hapo hawatapokelewa na nafasi zao zitajazwa na wengine wenye sifa ambao walikosa nafasi.

“Wanafunzi wote waliochaguliwa wanatakiwa waripoti katika vyuo vyao kuanzia tarehe 20 mwezi huu hadi 6 Oktoba mwaka huu.  Watakaoripoti baada ya hapo hawatapokelewa na nafasi zao zitajazwa na wanafunzi wengine walioomba ambao wana sifa ila walikosa nafasi,” amesisitiza Dkt. Akwilapo.

Aidha, Dkt. Akwilapo amesema serikali inatambua kuwepo kwa wanafunzi wengi waliokosa nafasi za kujiunga na masomo katika kozi mbalimbali na hivyo ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kufungua dirisha dogo la udahili kwa siku 14 kuanzia tarehe 7 Septemba ili wanafunzi waliokosa nafasi za masomo katika kada mbalimbali waweze kutumia fursa hiyo.


“Wizara inatambua kuwepo kwa idadi kubwa ya waombaji waliokosa nafasi katika awamu hii kutokana aidha na ushindani au kutofanya uchaguzi sahihi wa kozi hivyo wizara inaiagiza NACTE kufungua dirisha dogo la udahili kuanzia leo tarehe 7 hadi 21 Septemba ili kuwapa nafasi waombaji waliokosa nafasi katika programu mbalimbali waweze kufanya uchaguzi upya,” amesema Dkt. Akwilapo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (katikati) akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma. Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Avemaria Semakafu (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Udahili wa Baraza la Taifa la Ufundi (NACTE), Twaha Twaha.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu akiongea katika mkutano huo amesema baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakichagua kozi ambazo hawana sifa zinazohitajika.  Amewaasa waombaju kuzingatia sifa za kozi ili kuepuka kuenguliwa kwani masharti yanayowekwa kuhusu sifa hayabadilishwi.

“Utakuta kwa mfano mtu ana ufaulu mzuri wa alama A hadi C katika masomo ya lugha, badala ya kuchagua kozi zinazotaka ufaulu wa lugha yeye atachagua kozi za masomo ya sayansi ambayo kapata alama D, matokeo yake anajikuta hachaguliwi katika kozi alizoomba,” amesema Dkt. Semakafu.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Udahili wa NACTE, Twaha Twaha amewatahadharisha waombaji hasa wa kozi za afya kuhakikisha kuwa wamefaulu vizuri katika masomo ya sayansi kwani ndio sifa ya msingi katika udahili wa kozi hizo.


“Katika kozi za afya vigezo vinaangalia masomo, mfano mwanafunzi anayetaka kusoma clinical medicine au nursing, anatakiwa awe na ufaulu wa alama D katika masomo ya Physics, Chemistry na Biology.  Sifa zote hizi zipo katika kitabu cha Mwongozo wa Udahili ambacho kinapatikana kwenye tovuti ya NACTE ambayo ni www.nacte.go.tz,” amesema Twaha.

Alhamisi, 29 Agosti 2019

TAARIFA KWA UMMA


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
COMMONWEALTH SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE UNITED KINGDOM 2020

The Ministry of Education, Science, and Technology as a Nominating Agent in the Country for the Commonwealth Scholarships is inviting applications from qualified Tanzanians for Masters and Doctoral Degree Tenable in the United Kingdom for the academic year 2020.

The Scholarship includes:

  • One year taught Master Degrees
  • Doctoral degree of up to three years duration.

 Qualification:
i.        Applicants must be holders of bachelor or masters degrees.
ii.      Applicants for master’s degree must have a bachelor degree with a GPA of not less than 3.5.
iii.    Applicants for PhD must have a master’s degree with a GPA of not less than 4.0.

Mode of application:



  • It is important that applicants should read and understand all instructions when filing the application forms, and all applicants must attach all the required attachments such as certified copies of academic certificates, transcripts, and birth certificates and submit them online through the above link;

  • All applicants must ensure that, referees submit reference letter on time;
  • Applicants who are employees must attach letters from their employers conforming that, if granted scholarship will be allowed to utilize these opportunities;
  • In order to be nominated, all applicants must submit the filled application forms accompanied with the attached certified photocopies of the academic certificates to the address below before 20th November 2019.


        Permanent Secretary,
        Ministry of Education, Science and Technology,
        Government City,
        Mtumba Block,
        Afya Street,
        P.O. Box 10,
        40479 DODOMA. 

Alhamisi, 22 Agosti 2019

BENKI YA DUNIA YAPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUTOA KIPAUMBELE KWENYE SEKTA ELIMU


Benki ya Dunia imepongeza Serikali ya Tanzania kwa kutoa kipaumbele  kwa sekta ya Elimu na kwamba ni moja kati ya nchi zilizofanikiwa sana katika kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata nafasi hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa jijni dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia ukanda wa nchi za Africa Anne Kabagambe alipofanya ziara katika shule ya Sekondari Kibasila akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari Kibasila ya Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati alipofanya ziara katika shule hiyo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe.

Mkurugenzi huyo ametembelea shule ya Kibasila kwa sababu Benki ya Dunia inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika juhudi zinazofanywa katika sekta ya elimu ikitambua kuwa elimu ni ndio chimbuko la maendeleo katika katika nchi yoyote.

Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amesema Benki ya Dunia imekuwa ikishirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo  ikiwemo mradi wa Elimu unaojulika kama Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) ambapo Benki ya Dunia imetoa dola za kimarekani milioni 202 katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2014 na unategemewa kumalizika mwaka 2021.
Walimu wa shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati alipotembelea shule hiyo akiwa na ugeni kutoka Benki ya Dunia.

Waziri Ndalichako amesema kupitia mradi huo takribani Sh bilioni 141 zimeshatumika kwa ajili ya kukarabati shule kongwe 62, kujenga vyumba vya madarasa 2,876, matundu ya vyoo 6,558, nyumba za walimu 59, mabwalo 76, majengo ya utawala 16, Mabweni 533 kwa ajili ya kuwaepusha watoto wa kike na changamoto za mbalimbali, pamoja na kujenga mifumo ya maji safi kwenye baadhi ya shule ambazo hazikuwa na vyanzo vya maji.

Aidha Waziri Ndalichako alisema kwa upande wa Shule ya Sekondari Kibasila  shilingi milioni 900 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020  kwa ajili ya ukarabati na tayari wataalamu  wameanza kufanya tathmini ya majengo ya shule hiyo ambayo ukarabati wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe akizungumza na walimu wa shule ya sekondari Kibasila wakati alipotembelea shule hiyo. Ameipongeza serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye sekta ya elimu.

Awali akitoa taarifa ya shule Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibasila Yasinta Matilya amesema moja ya changamoto inayokabili shule hiyo ni utoro wa wanafunzi unaotokana na changamoto za kifamilia ikiwemo watoto kulelewa na mzazi mmoja, kipato duni, umbali wa makazi ya wanafunzi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanafunzi wa shule hiyo wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa saikolojia watakaowasaidia kujitambua ikiwa ni pamoja na kuwajengea mabweni ili kuepukana na vishawishi vya barabarani pamoja na usumbufu wa usafiri wa unaopelekea wanafunzi kuacha shule.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Anne Kabagambe mara baada ya kuhitimisha ziara katika shule ya sekondari kibasila iliyoko jijini Dar es Salaam.



Jumatatu, 19 Agosti 2019

WAZIRI NDALICHAKO AWAASA WANAFUNZI WALIOPATA UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU NCHINI CHINA KUWA MABALOZI WAZURI


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amewaasa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya Elimu ya juu nchini China kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania nchini humo.


Waziri Ndalichako amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa China nchini.


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam.
Jumla ya wanafanzi 61 wamepata ufadhili wa masomo kwa Shahada za  Uzamili na Uzamivu katika fani za Afya, Uhandisi, Utabibu , TEHAMA na Mazingira.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiteta jambo na Balozi wa China nchini Wang Ke.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Balozi wa China nchini Wang Ke zawadi ya picha inayoonesha baadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi za Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China.