Jumatatu, 27 Machi 2017

KATIBU MKUU AKAGUA UJENZI WA CHUO CHA VETA, MKOANI MOROGORO.

Katibu mkuu wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi ametembelea na kukagua ujenzi unaoendelea wa majengo ya chuo cha Veta kilichopo kihonda  mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Tarishi amekagua  jengo la utawala na majengo mawili ya karakana ikiwemo karakana ya umeme wa magari na karakana ya  ufundi seremala, na kuwa ujenzi wa majengo hayo  kwa hivi sasa uko katika hatua za kupauliwa.







Ijumaa, 24 Machi 2017

NAIBU KATIBU MKUU AFUNGA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU

Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard akifunga kongamano la siku tatu la wadau wa Elimu waliokutana kuzungumzia masuala ya uongozi na usimamizi wa masuala ya Elimu katika karne ya 21 lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Taasisi ya kuendeleza Elimu Afrika Mashariki.



UZINDUZI WA MAKTABA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt Leonard Akwilapo akizindua maktaba ya Makumbusho ya Taifa Baada ya kupokea vifaa vya maktaba hiyo ikiwa pamoja na vishikwambi (TABLETS  kutoka kwa  Serikali ya  Watu wa Korea kupitia mradi wa THANK YOU SMALL LIBRARY.





Jumatano, 22 Machi 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII IKIKAGUA JENGO LA TEACHING TOWER LILILOPO DIT.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Maendeleo na huduma za jamii wakikagua jengo la kufundishia, ambalo ndani yake kuna ofisi, chumba cha ujasiriamali, na vyumba vya madarasa, (Teaching Tower)








Jumanne, 21 Machi 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAENDELEO NA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA MLOGANZILA.

Kamati ya bunge ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Maendeleo na huduma za jamii, Peter Serukamba na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, Naibu waziri Mhandisi Stella Manyanya na Naibu katibu Mkuu Dkt. Leonard Akwilapo, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua mradi wa MLOGANZILA chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).








Jumapili, 19 Machi 2017

NAIBU WAZIRI AZINDUA VISHKWAMBI.

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amewataka wadau wa Maendeleo ndani na nje ya nchi kuangazia maeneo ya vijijini kufuatia miradi mbalimbali ya maeneo kuangazia maeneo ya mijini zaidi.

Mheshimiwa Manyanya ametoa kauli hiyo hii leo katika shule ya msingi ya Olympio wakati akikabidhi vishkwambi (tablets)ambavyo vinatarajiwa kusambazwa katika shule mbalimbali za jijini Dar es salam.

Mhandisi Manyanya amesema umefika wakati sasa mradi wa majaribio kama huu wa Elimu kwa njia ya TEHAMA upelekwe hadi maeneo ya vijijini na siyo kubakia kwenye maeneo ya mijini pekee.

Naibu Waziri manyanya pia amewataka walimu kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa hasa ya kuwafundishia wanafunzi.

 





Ijumaa, 3 Machi 2017

WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WA VYUO VYA MAENDELEO YA WANANCHI (FDCs).

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya wananchi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi Kwa uadilifu, ubunifu, na weledi wa hali ya juu ili vijana wanamaliza kwenye vyuo hivyo wawe na ujuzi na uwezo wa kujiajiri wenyewe.

MAMBO YA MSINGI AMBAYO WAKUU WA VYUO  VYA FDCs WAMETAKIWA KUZINGATIA;
1-KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
2- WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU
3- WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA MSHIKOMANO
4- WAMETAKIWA KUWA WAADILIFU
5- WAMETAKIWA KUTUMIA NA KUTHAMINI RASILIMALI