Jumatano, 10 Aprili 2019

SERIKALI YA TANZANIA NA ROMANIA WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA ELIMU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Romania Daniela Gitman pamoja na ujumbe wa Kamati ya Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Romania na kukubaliana kushirikiana katika sekta  ya elimu.

Akizungumza na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Ndalichako jijini Dodoma, Balozi Gitman amesema  hii ni mara ya kwanza kwa nchi yake kuingia katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa lengo la kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Balozi Gitman amesema nchi yake imeiteua Tanzania kuwa chimbuko la kuanzishwa kwa  ushirikiano kati Serikali ya Romania na nchi za Afrika Mashariki kwenye maeneo mbalimbali ambapo wanaanza na sekta ya elimu na baadaye wataaangalia sekta za utalii na biashara.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Naibu Katibu Mkuu Prof. Prof. James Mdoe, Kaimu Mkurgenzi Elimu ya Juu na Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Dkt. Kipanyula wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima kutoka Romania na  Wajumbe wengine.

Katika Kikao hicho wamekubaliana kutoa ufadhili wa masomo ya shahada za juu kwa wahadhiri na wataalamu katika Vyuo Vikuu vya Tanzania katika fani ambazo Umoja wa Wakuu wa Vyuo Vikuu Tanzania utapendekeza kulingana na vipaumbele vya nchi.

Pamoja na kufadhili wahadhiri, Wamekubaliana kupitia Vyuo Vikuu kuanza utaratibu wa kubadilishana uzoefu na utaalamu “fellowships”, ambapo wahadhiri kutoka Tanzania wataenda Romania na Romania kuja Tanzania kwa vipindi vifupi vifupi.

Waziri Ndalichako ameishukuru serikali ya Romania na kuahhidi kushirikiana nao katika kuendeleza sekta ya elimu na kuuwataka Umoja wa Wakuu wa Vyuo Vikuu nchini kuhakikisha wanakamilisha kuandaa makubaliano ya ushirikiano huo pamoja na taratibu za utekelezaji wa ushirikiano huo.

Katika hatua nyingine Romania imetoa fursa ya kufadhili masomo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi 5 katika kila fani itakayopendekezwa kusoma katika Vyuo Vikuu nchini humo. Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na vyuo vikuu wataratibu upatikanaji wa wanufaika.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe na  Mkurugenzi wa Elimu Juu Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia na Wakurugenzi wa Wizara hiyo ambapo utakelezaji wa makubaliano hayo unatarajiwa kuanza mara baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano na programu za maunzi kwa wanufaika zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba Mwaka huu.



UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY


SCHOLARSHIP TENABLE IN THE GOVERNMENT OF INDONESIA 2019-2020
 
Call for Application
The General Public is hereby informed that, the Kemitraan Negara Bekembang (KNB), offers scholarship opportunity to Tanzanian to study different programme in various University in Indonesia.

Mode of Application
All interested candidates should apply through an online application found in the following link: http://www.knb.ristekdikti.go.id/ .

Furthermore, information visit the following links: file:///E:/KNB_Application_Guidelines_2019.pdfand http://www.knb.dikti.go.id/
Other require documents
Recommendation letter is issued by the Embassy and is mandatory; it can be required by submitting the required documents (invitation letter, Passport or birth certificate, academic certificates and academic transcript) to the Embassy of the Republic of Indonesia or via email: zefanyatodoan@gmail.com
The online application should be completed no later than April 12th, 2019
Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P .O. Box 10,
40479 Dodoma.

Jumatatu, 8 Aprili 2019

NORWAY NA TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA ELIMU


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia kuendeleza ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifanya mazungumzo na Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen kuhusu Sekta ya Elimu.

Waziri Ndalichako ameishukuru serikali ya Norway kwa kuendelea kufadhili sekta ya elimu kupitia Mfuko wa Global Partnership for Education (GPE ) na amemuhakikishia Balozi Jacobsen kuwa fedha zote zinazotolewa na kupitia mpango huo zitatumika kama ilivyokusudiwa.

Waziri Ndalichako amevitaja vipaumbele vya ufadhili huo kuwa ni masuala ya uthibiti ubora wa shule, ununuzi wa  vitabu na kutoa  mafunzo kwa walimu walio kazini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen pamoja na viongozi wengine Mjini Dodoma

Kwa upande wake Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika elimu na kueleza kuwa wanaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa uanzishaji Kituo cha kufuatilia Hewa ya Ukaa katika  Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).

Kituo hicho kinafadhiliwa na Serikali ya Nchi ya Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiagana na Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen

Jumatatu, 1 Aprili 2019

WAZIRI WA ELIMU AZINDUA UKUMBI WA KISASA WA MIHADHARA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amezindua ukumbi wa mihadhara wa kisasa katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere uliojengwa mapato ya ndani ya Chuo hicho.

Akizundua ukumbi huo wa Mihadhara kigamboni jijini Dar es salaam Waziri Ndalichako amepongeza Bodi ya Utawala na Uongozi wa Chuo hicho kwa kusimamia vema matumizi ya fedha zinazotokana na Mapato ya ndani na kutumia kutekeleza miradi yenye tija kwa Chuo na Taifa kama ilivyofanyika katika ujenzi wa Ukumbi huo na pia amewataka uongozi kusimamia Dira na Dhima ya uanzishwaji wake kwa kujikita katika kutoa mafunzo ya Uongozi, Utawala na Maadili.

Waziri Ndalichako amewapongeza Watendaji wa Chuo kwa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Mradi huo hadi kufikia hatua ya kukamilisha japo kwa kuchelewa kwa karibu miezi tisa.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa Ukumbi mpya wa Mihadhara uliyojengwa katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni uliojengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Chuo hicho.

“ nimefurahishwa na kazi hii nzuri iliyofanyika hapa, kwakweli ni jengo zuri lenye ubora wa hali ya juu na ambalo litawafanya wanafunzi kuongeza ari ya kujifunza na ninategemea kuona jengo hili likituzwa vizuri ili litumike kwa miaka mingi likiwa na ubora uleule”. Amesisitiza Ndalichako

Aidha Ndalichako amezitaka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuthamini na kutumia vizuri mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutekeleza mipango na Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika taasisi hizo ili kuleta maendeleo ya haraka badala ya kuzitumia fedha hizo kwa matumizi mengine yasiyo na tija.

Wakati huo amewataka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ni wakandarasi  wa ujenzi wa Ukumbi huo kukamilisha miradi mingine iliyo chini ya Wizara ya Elimu ikiwemo ukarabati wa shule Kongwe mfano Kibaha Sekondari, Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea pamoja na ujenzi wa Hosteli na miundombinu mingine katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyereer Stepen Wasira wakati wa uzinduzi wa Ukumbi wa Mihadhara uliyojengwa katika Chuo hicho.



Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo hicho Stephen Wasira, amesema Chuo hicho kimejipanga kuhahakisha kinatoa elimu bora na wahitimu walio bora wenye weledi hasa katika eneo la uongozi na utawala ili kuenzi fikra na maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alieanzisha chuo hicho Mwaka 1961 kwa lengo la kuandaa viongozi na watawala.

Awali, Mkuu wa Chuo Prof. Shadrack Mwakalila akitoa taarifa ya mradi amesema jengo hilo limegharimu zaidi ya Shilingi za Tanzania Bilioni 1.1  na kwamba lina uwezo wa kuchukua wanafunzi 330 kwa wakati mmoja. Ameongeza kuwa pamoja na ukumbi wa Mihadhara jengo hilo lina ofisi nane za wahadhiri na mifumo ya kisasa ya sauti.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Bibi Thabita Siwale Waziri wa kwanza wa Elimu mwanamke Tanzania ambae pia alipitia mafunzo katika Chuo hicho aliyehudhuria hafla ya uzinduzi wa Ukumbi wa Mihadhara uliyojengwa katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.