Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Mkinga
akimkabidhi  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish 
baadhi ya nyaraka mbalimbali zinazohusu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
ambavyo sasa vitakuwa vikiendeshwa na kusimamiwa  na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Saimon Msanjila. 
Katibu
Mkuu Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish akizungumza na watendaji
wa Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia na Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto  wakati wa  makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara.



 
 



