Ijumaa, 26 Aprili 2019

WAZIRI NDALICHAKO AIPONGEZA CHINA KWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ameipongeza Jamhuri ya Watu wa China kwa kuimarisha ushirikiano  na  Tanzania hususan katika sekta za Elimu, Biashara na Ujenzi wa miundombinu.

Waziri Ndalichako ametoa pongezi hizo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na China ambapo amesema kuwa mahusiano kati ya nchi hizo mbili ni ya muda mrefu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Watu wa China na Jamhri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Prof. Ndalichako amesema mchango wa nchi hiyo kwenye maendeleo ya Tanzania ni dhahiri akitolea mfano  wa ujenzi wa Reli ya TAZARA pamoja na ujenzi wa viwanda mbalimbali vya nguo nchini.

Prof. Ndalichako amesema pia China imeendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa kubadilishana uzoefu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Wag Ke (Hayupo pichani) katika sherehe za kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda, Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara, na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi  za umma na binafsi nchini. 

Alhamisi, 25 Aprili 2019


UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY
SCHOLARSHIP TENABLE IN THE GOVERNMENT OF PAKISTAN
2019-2020
Call for Application
The General Public is hereby informed that, the Government of Pakistan has offered scholarships opportunity to Tanzanian to study Master’s degree programme in the Public Universities.  Eligible candidates may apply in field of Social Sciences, Gender Studies, Arts & Humanities, Management and Business Education, Agriculture and Veterinary Sciences, and Natural Sciences/Physical Sciences.

For further information, Procedure for application, Fields of study, Financial breakdown, Eligibility criteria, Required documents, Universities and Admission procedure please visit the following link:http://www.hec.gov.pk/english/scholarshipsgrants/ARL-FS/CWLDC/Pages/default.aspx
The application should be completed no later than May 15th, 2019.
Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P .O. Box 10,
40479 Dodoma.

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY


  STUDY OPPORTUNITY OFFERED BY THE ORGANIZATION FOR WOMEN IN SCIENCE FOR THE DEVELOPING WORLD (OWSD-EARLY CAREER FELLOWSHIP) 2019/2020

Call for Application
The General Public is hereby informed that, Organization for Women in Science for the Developing World (OWSD) has offered scholarships opportunity to Tanzanian women. The OWSD Early Career fellowship is a prestigious award of up to USD 50,000 offered to women who have completed their PhDs in Science, Technology, Engineering and Mathematics (STEM) subjects and are employed at an academic or scientific research institution in one of the listed Science and Technology Lagging Countries (STLCs). The OWSD Early Career fellows will be supported to establish an environment at their institution where they can maintain an international standard of research and attract scholars from all over the world to collaborate.

Mode of Application

Note: The official language for the application is English; however, all information about the programme is also available in French at: https://bit.ly/2IKPfRZ.

Submission
Online application must be submitted not later than 30th April, 2019.

Issued by:
Permanent Secretary,
Ministry of Education, Science and Technology,
University of Dodoma,
College of Business and Law,
Block 10,
P .O. Box 10,
40479 DODOMA.

Jumatano, 24 Aprili 2019

BARAZA LA WAFANYAKAZI WIZARA YA ELIMU LAKUTANA KUJADILI MWELEKEO WA BAJETI KWA MWAKA 2019/20.


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Filisi Nyimbi amesema serikali ya awamu ya tano imeweka misingi imara itakayowezesha kila mtanzania kupata elimu iliyo bora na yenye tija kwa Taifa ili kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo mwaka 2025.

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoojia unaofanyika mkoani Mwanza na kusisitiza kuwa Wizara hiyo imepewa jukumu la kutunga sera, kuandaa na kusimamia miongozo mbali mbali ya Elimu itakayowezesha Elimu inayotolewa nchini kuwa bora.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa wameshikana mikono wakati wa kiimba wimbo wa “SOLIDARIRY” kuashiria umoja, mshikamano na upendo katika utekelezaji wa majukumu yao
 


Dkt. Nyimbi amesisitiza kuwa ili kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano kila mtumishi ana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi wa hali ya juu.

Dkt. Nyimbi ameipongeza Wizara ya Elimu kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika Shule za Sekondari, Vyuo vya Ualimu, Elimu ya Juu, Vyuo vya Ufundi,  na Vyuo vya Maendeleo ya wananchi (FDCs) lengo likiwa ni kuweka mazingira bora ya kielimu katika kuandaa vijana wenye sifa katika kujenga uchumi wa nchi.Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Filisi Nyimbi Akizungumza na washiriki katika Mkutano wa  26 wa  Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria.


Pia ameipongeza Wizara kwa kuendelea kuimarisha na kuboresha  idara ya Uthibiti Ubora wa shule kwa kununua magari ili idara hiyo iendelee kukagua shule na kutoa ushauri wa kitaalamu  na kitaaluma.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe amesema pamoja na mambo mengine kikao hicho kitapitia utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2018/19 na kujadili mwelekeo wa bajeti kwa mwaka 2019/20.Mgeni rasmi Dkt. Filisi Nyimbi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na  washiriki wa Mkutano wa 20 wa Baraza la Wafanyakazi wakiwa kwenye picha ya pamoja. Kikao kazi hicho kimefanyikia mkoani Mwanza.
 


“Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa majukumu yake kwa lengo la kuboresha sekta ya Elimu hapa nchini, hivyo niwaase watendaji wote kuendelea kufanya kazi kwa kufauta kanuni, taratibu na sheria zinazosimamia utendaji katika maeneo yenu ya kazi,”alisisitiza Prof. Mdoe.

Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 120 kutoka Wizara ya Elimu na wajumbe kutoka Chama cha Walimu Tanzania ( CWT ) na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na  Afya (TUGHE).   Kauli mbiu ya Mkutano huo wa 26 wa baraza la wafanyakazi ni: “Elimu bora na Uwajibikaji wa pamoja ni Chachu ya Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda Tanzania”Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 26 wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia hotuba ya  mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika Jijini Mwanza