Jumanne, 6 Desemba 2016

Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakutana Dar


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Serikali ya Canada  na Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira  unaendesha warsha ya siku tatu inayojadili Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi  kwa kushirikisha mfumo shirikishi, mafunzo ya kuendeleza ujuzi, na Masuala ya Jinsia. 

Warsha hii inayofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii (Bustani) inalenga kusaidia uanzishwaji wa mfumo wa kuongeza  ushirikiano miongoni mwa watendaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi sekta nchini.

Wadau mbalimbali wameshirikishwa katik warsha hii ambayo imewaleta pamoja wadau wa elimu ya ufundi na wawakilishi mbalimbali wakubwa, mashirika mbalimbali yanayotoa elimu na mafunzo, watu binafsi, waajiri na vyama vya waajiri, soko la ajira mashirika ya habari na mashirika ya kiraia ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi ya kuwezesha wanafunzi wanaohitimu katika  Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi anakuwa na ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa.

:   Mshauri Mwandamizi wa Ufundi na mwakilishi wa Vyuo na Taasisi  zinazosaidia vyuo na Vyuo vya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi Canada Dr. Alan Copeland  (aliyesimama) ambaye kwa sasa anasimamia Mradi wa Kuboresha Mafunzo ya Ujuzi kwa ajili ya Ajira  nchini akizungumza katika warsha ya siku tatu ya wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi inayofanyika jijini Dar es Salaam inayojadia masuala mbalimbali kuhusu sekta hiyo.





Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu ya Ufundi na Mafunzo Ufundi Stadi. Warsha hii imewaleta pamoja wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuweza kujadili kwa pamoja jinsi inavyoweza kufanya vijana kuweza kujiajiri na kuajiriwa wakiwa na ujuzi stahiki.

Waziri wa Elimu hakutana na Ujumbe wa Benki ya Dunia



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na wajumbe kutoka Benki ya Dunia waliofika wizarani kuongea naye masuala mbalimbali ya Elimu na jinsi ya benki hiyo itakavyoendelea kusaidia sekta ya elimu nchini wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Sajitha Bashir, Cornelia Jesse na Gayle Martin kutoka Benki ya Dunia.
Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Elimu aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya elimu ambayo imekuwa chachu ya kuleta maboresho katika sekta ya elimu nchini. Hivyo amewaomba kuendelea kusaidia kutoa misaada mbalimbali katika elimu ili kuhakikisha inaendelea kuboreshwa na kuwapa fursa watoto waengi wa Kitanzania kupata elimu iliyo bora.
Naye Mjumbe kutoka Benki ya Dunia Sajitha Bashir amemuhakikishia Waziri wa Elimu kuwa Benki ya Dunia itaendelea kufadhili miradi ya Elimu nchini pale itakapoitajika. Aidha, alisisitiza kuwa miradi yote inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ni lazima itoe matokeo yanayokusudiwa

Waziri wa Elimu azindua mashindano ya Ujuzi


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizungumza katika uzinduzi wa Mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.




Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mmoja wa washiriki wa mashindano ya Ujuzi Afrika Mashariki (East Africa Skills Competition) yanayofanyika katika Chuo cha Ufundi cha Dare es Salaam.

Balozi wa Uingereza amtembelea waziri wa Elimu na kufanya mazungumzo



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiongea na Balozi wa Uingereza Sarah Cooke nchini aliyefika ofisini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu Elimu nchi. Aidha, katika mazungumz0 hayo Waziri aliishukuru Uingereza kwa kusaidia na kufadhili miradi mbalimbali ya Elimu nchini

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiangalia baadhi ya taarifa kuhusu vitabu vya lugha ya Kiingereza vinavyoandaliwa na DFID  kwa ajili ya kusambazwa kwa shuleni. Vitabu hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi pamoja na walimu, pichani ni Balozi wa Uingereza Sarah Cooke na Mwakilishi wa DFID Tanya Zebioff


Alhamisi, 1 Desemba 2016

China yakabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia


Serikali ya China imekabidhi vitendea kazi kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuwezesha wizara kufanya kazi kwa weledi. vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Naibu Katibu Mkuu Prf. Saimon Msanjila ofisini kwake na Liu Yun

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Liu Yun alimwelezea Naibu Katibu Mkuu kuwa wanajisikia faraja kubwa kukabidhi vifaa hivyo kwa wizara kwani China na Tanzania zimekuwa zikishirikiana kwa karibu sana katika sekta ya elimu hasa katika upande wa elimu ya juu.

Vitendea kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na Dell desk compture 6, mashine ya kudurufu moja, scanner moja, video camera moja na komputa mpatako 10 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano

Ushirikiana huo umewezesha serikali hizi mbili kuweza kubadilishana wanafunzi wa elimu ya juu katika fani mbali mbali. Pia alimuelezea uanzishwaji wa mafunzo ya lugha ya kichina katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam ambapo alisema hii ni ishara tosha ya ushirikiano uliotukuka.

Naye Naibu Katibu Mkuu alimshukuru Yun kwa msaada huo wa vitendea kazi ambapo alimuahidi kuwa vitafanyia kazi iliyokusudiwa na kuhakikisha kwamba inaongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi wanaofika ofisi hapo kupata huduma mbalimbali za kielimu.

Baadhi ya vtendea kazi vilivyotolewa na serikali ya China kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuboresha na kurahisisha utendaji kazi wa watumishi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi 


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakisoma na kujadiliana nyaraka mbalimbali za vifaa wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila  na Mwakilishi wa Serikali ya China Liu Yun wakiweka saini makubaliano ya kupokea vifaa vilivyotolewa na China wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi