Jumatano, 22 Juni 2016JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA 

TANGAZO

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA MWAKA 2016

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Mwaka 2016 yalianza  tarehe 16 Juni na yatafikia kilele tarehe 23 Juni.  Kwa mwaka huu 2015/16 imeamuliwa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yafanyike kwa utaratibu ufuatao:

(i)                 Tarehe 22/06/2016 kuanzia Saa 7:00 hadi 9:00 mchana watumishi wote wenye matatizo sugu yanayowakabili wafike Ofisini kwa Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu (S) kueleza matatizo yao ili yaweze kushughulikiwa.
 
(ii)              Tarehe 23/06/2016 kuanzia Saa 5:00 asubuhi hadi Saa 9:00 mchana wateja wenye kero wafike Ofisini kwa Katibu Mkuu au Naibu Katibu Mkuu (S) ili waweze kusikilizwa kero zao.
 
UTAWALA
21/06/2016