Jumatatu, 20 Februari 2017

Serikali za Tanzania na China zatia saini ujenzi wa Chuo cha VETA Kagera 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi na Mwakilishi wa Masuala  ya Uchumi na Biashara ya Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong wametiliana saini makubaliano ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA kitakachojengwa  Gera mkoani kagera


Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  Maimuna Tarishi akibadilishana hati za makubaliano (MOU) na Mwakilishi wa Masuala  ya Uchumi na Biashara wa Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong mara baada ya kutiliana saini.

Alhamisi, 16 Februari 2017

Mkutano wa SDGs4 unaendelea leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini DSM nchini Tanzania

Mawaziri kutoka nchi Kumi tatu, wawakilishi, mabalozi na wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri wa elimu katika mkutano wan chi za Ukanda wa Afrika Mashariki wa akuaanisha changamoto zinazofanana katika mfumo wa  elimu ili kubadilishana uzoefu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo. Mkutano huo unatarajiwa kuitimishwa leo jioni.Mawaziri kutoka nchi Kumi tatu, wawakilishi, mabalozi na wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri wa elimu katika mkutano wan chi za Ukanda wa Afrika Mashariki wa akuaanisha changamoto zinazofanana katika mfumo wa  elimu ili kubadilishana uzoefu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo. Mkutano huo unatarajiwa kuitimishwa leo jioni.MKUTANO WA NCHI 13 ZA UKANDA WA A. MASHARIKI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDFELEO ENDELEVU SDGs4 YA ELIMU 2030

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifungua mkutano wa nchi kumi na tatu za ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu utekelezaji wa Malengo yaMaendeo Endelevu SDGs4 ya elimu 2030 ambao unafanyika tarehe 15/02/2017 hadi tarehe 16/02/2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Waziri wa Elimu amebainisha malengo ya mkutano huo kuainisha changamoto zinazofanana na kubadilishana uzoefu wa namna wa kukabiliana na changamoto hizo, ambapo kwa pamoja wanahitaji  uwepo kwa elimu jumuishi yenye usawa bila kujali wanakotoka.

Jumatatu, 6 Februari 2017

Waziri wa Elimu atoa vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika sekta ya Elimu nchini.


    Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni Mia Saba na Nne, Mia Sita Ishirini na Saba Elfu na Mia Nane Hamsini Na Sita (704,627,856/=) kwa Halmashauri ya kwanza ya Kaliua Kati Ya Halmashauri zote Nchini zilizoshindanishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [ (P4r).
      Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikabidhi cheti cha ushindi kwa Halmashauri ya Kaliua iliyopata ushindi wa kwanza Kati ya Halmashauri zote Nchini zilizoshindanishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [ (P4r).