Jumanne, 30 Septemba 2014


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING

GOVERNMENT SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE REPUBLIC OF KOREA FOR THE YEAR 2015

The Ministry of Education and Vocational Training is inviting application from qualified Tanzanians for the undergraduate degree programme (hereafter called 2015 undergraduate GKS”)   to be  conducted in the Republic of Korea for the academic year 2015- 2020

Qualifications
Prospective candidates must meet the following qualifications:-
·         Applicants must have passed their Advanced Certificate of Secondary Education Examination with an average of B+ grade or above;
·         Applicants must not be older than 25 years by March, 1st , 2015; and
·         Applicants must not at any time have ever received Korea Government Scholarship for undergraduate studies


Mode of Application
(a)   All application should be made using application forms from the Website http://www.studyinkorea.go.kr;
(b)   Applicants can apply for all other programmes except those which are exceeding four years duration (eg. medicine, dentistry, pharmacy, architecture etc); and
(c)    Application forms should be filled as per guidelines and be attached with all necessary attachments as stipulated in the checklist.
Completely filled application forms should be submitted to the address below before 15th October, 2014


The Permanent Secretary,
Ministry of Education and Vocational Training,
 
P.O. Box 9121,
DAR ES SALAAM

Jumanne, 23 Septemba 2014

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING

COMMONWEALTH SCHOLARSHIPS TENABLE IN THE UNITED KINGDOM FOR THE YEAR 2015
The Ministry of Education and Vocational Training as a nominating agent in the country for the Commonwealth scholarships in inviting applications from qualified Tanzanians for Masters and Doctorate degrees tenable in the United Kingdom in the year 2015.

The Scholarships include:
·         One year taught masters courses of equivalent degrees.
·         Doctorate degrees of up to three years duration.

Qualifications
1.      Applicants must be holders of bachelor of masters degrees;
2.      Applicants for masters must have bachelor degrees of GP A not less than 3.5; and
3.      Applicants for Doctorate degrees must have a B Grade Masters degrees or a GPA 4.0 or above at Masters level.

Mode of Application:
·         All applications should be made directly to the Commonwealth Secretariat and should be online using the following link:http://bit.ly/cscuk-apply.

·         It is important that applicants should read and understand all given instructions when filling the application forms, and should attach all necessary attachmentssuch as certified copies of academic certificates, transcripts, birth certificates and submit online through the above mentioned link.

All applicants who wish to be nominated by the Ministry of Education and Vocational Training, should print one hard copy of completely filled application form, attach with certified photocopies of academic certificates, transcripts and birth certificates and submit them to the address below before 31st October, 2014.

The Permanent Secretary,
Ministry of Education and Vocational Training,
P.O. Box 9121,

DAR ES SALAAM.

Alhamisi, 11 Septemba 2014

WAZIRI KAWAMBWA AWAAGIZA WAMILIKI WA SHULE KUFANYIA KAZI RIPOTI ZA UKAGUZI.



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa amewataka Wakaguzi wa Shule kuhakikisha ripoti wanazotoa kwa wamiliki wa shule, shule, bodi za shule na kwa walimu baada ya ukaguzi shuleni  zinafanyiwa kazi mara moja ili kupunguza changamoto zinazoikabili sekta ya Elimu. 

Mhe. Dkt Kawambwa aliyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Ukaguzi kitaifa iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE).
 “Wamiliki wa shule mnapaswa kufanyia kazi ripoti zinazotolewa na Wakaguzi wa Shule badala ya kuziweka katika makabati,  lazima tuhakikishe  mapungufu yote yaliyobainishwa yanapatiwa ufumbuzi mara moja ili kuninua ubora wa Elimu.”  Alisema Dkt. Kawambwa.

Aidha, amesema ni aibu kwa Wakaguzi wa Shule kuendelea kukagua na kukutana na changamoto zilezile ambazo walikutana nazo wakati walipofanya ukaguzi kwa mara ya kwanza na kuzitolea ripoti kwa wamiliki wa shule na bado hazifanyiwi kazi..

Hata hivyo Dkt. Kawambwa, aliwambia  wadau wa Elimu kuwa zipo changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya Elimu, ambazo ni pamoja na uhaba wa rasilimali watu, rasilimali fedha, utendaji na usimamizi mbovu, msongamano wa wanafunzi darasani, utoro, uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati, uhaba wa Majengo,  na uhaba wa maabara.

Waziri amesema changamoto nyingi katika sekta ya Elimu zinatokana na ukosefu wa ushirikiano kati ya Wizara na wadau wa Elimu, na hivyo basi kuwaomba wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana kwa pamoja ili kuleta  mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu.

Dkt. Kawambwa amewataka wananchi na wadau wa Elimu kuwauliza wakaguzi wa shule, ni mara ngapi wamezikagua shule na wameshauri nini na je ushauri huo umezingatiwa na kufanyiwa kazi, yote hayo yanahitajika ili kufanikisha Mpango mpya wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN).

Waziri akiitimisha hotuba yake katika kongamano hilo la wiki ya ukaguzi aliwasihi wadau wa Elimu kuitumia vizuri kauli mbiu ya maadhimisho hayo inayosema “Ukaguzi Fanisi Na Endelevu Kwa Elimu Bora” kujadili kwa kina  mada zote  katika kongamano hilo zitakazo wasilishwa na wataalamu ili kupata matokeo yanayotarajiwa katika sekta ya Elimu nchini.












WAZAZI WATAKIWA KUSIMAMIA NIDHAMU YA WATOTO



Waziri wa Elimu na Mafunzo  ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa  amewataka  wazazi kusimamia ipasavyo maadili ya watoto wao ili waweze kufanikiwa na kufikia malengo  waliyojiwekea kitaaluma. Pia aliwataka kushirikiana na walimu katika kuhakikisha watoto wanakuwa na nidhamu ya kuridhirisha katika jamii inayowazunguka.   

Dkt Kawambwa alitoa wito huo katika mahafari ya kuwatunuku vyeti wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Msingi  Kongo iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani. Ambapo aliwataka walimu na wazazi kuhakikisha wanawasisitiza wanafunzi kutii sheria za shule kama vile uvaaji wa sare sahihi ya shule, kuheshimiana na utumiaji wa lugha nzuri.

“Wazazi tuna jukumu kubwa la kusimamia suala la maadili ya  watoto wetu. Hili ni suala ambalo huwezi kulitenanisha na mafanikio bora kitaaluma. Mara nyingi mtoto wenye nidhamu na maadili mema daima hufanya vizuri darasani na yule asiye na nidhamu huporomoka katika taaluma. Nasisitiza nidhamu na taaluma huenda pamoja, haiwezekani kuvitenganisha hata mara moja.” Alisisitizi Dkt. Kawambwa.
Aidha, aliwataka wanafunzi wote nchini wanaomaliza darasa la saba kujiandaa vyema kufanya Mitihani yao inayotarajiwa kuanza,  kujitahidi kutulia na kutumia vyema maarifa yote waliyopata kutoka kwa walimu wao. Aliwakumbusha kwamba watakapomaliza mitihani yao wasijisahau na kufikiri kuwa sasa elimu ndio basi bali watambue kuwa safari ya kutafuta elimu ndio inaanza.

Dkt Kawambwa aliwataka kutenga muda wa kujiandaa kwa masomo ya sekondari mara wanapomaliza mitihani yao ya darasa la saba. "Nawasihi muwe raia wema wenye kuwajibika katika jamii yote. Maisha sio lele mama! wekeni juhudi katika masomo, elimu ndio msingi bora wa maisha, msidanganyike hakuna njia ya mkato katika kufanikiwa katika maisha".  aliongeza Dkt. Kawambwa. 
Waziri Kawambwa aliwataka walimu wote nchini kutambua kuwa shughuli za kila siku shuleni zinahitaji juhudi za hali ya juu. Aliwataka kuboresha  zaidi utendaji kazi wao ili kufikia matarajio ya Taifa ya kuwa na  watu walioelimika na wenye uwezo wa kuhimili  changamoto zinazotokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Waziri aliwasisitiza walimu kukabiliana na changamoto zinzojitokeza katika sekta ya elimu kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea, badala yake kuhakikisha wanapanga mipango yao, wanajiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu na kubuni mikakati sahihi inayotekelezeka ambayo itawezesha kufikia malengo waliyojiwekea.  

Aidha, aliwashauri wazazi  kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika suala zima la kufanikisha matokeo mazuri ya ufaulu kuanzia madarasa ya awali, la kwanza hadi darasa la Saba. "Yote haya yanawezekana pale tutakapotekeleza wajibu wetu wa kusimamia vyema yale yote wanayofundishwa watoto wetu wanapokuwa shuleni. Watoto hupewa mazoezi mbalimbali (homework) na walimu wao ili wazifanye wanapokuwa nyumbani, ni jambo la msingi tukitenga muda kusimamia katika eneo hili. "

  Pia aliwataka wazazi kuhakikisha wanatimiza jukumu lao la kuwapatia watoto mahitaji muhimu yanayotakiwa shuleni.  Kwani mara nyingi utoro wa Wanafunzi shuleni huchangiwa sana wanafunzi wanapo shindwa kupatiwa mahitaji yao ya shule.

Aliwataka wanafunzi wanaobaki shuleni kujitahadi  kuzingatia Masomo. Kwani kipindi walichonacho shuleni ni kifupi sana, lakini ni kipindi  muhimu sana katika kuandaa maisha yao ya baadaye. Amewataka kuwasikivu, kutii sheria za shule, tekeleza majukumu yao wanayopewa katika masomo, kuepuka vitendo viovu katika jamii. Alwasihi kuwa na nidhamu inayopendeza machoni na mioyoni mwa wazazi, walezi na walimu wao. 

Shule ya Msingi Kongo ilianzishwa mwaka 1976 ikiwa na wanafunzi 38 na sasa ina wanafunzi 612 kuanzia Darasa la Awali hadi Darasa la Saba. Wanafunzi 72 wanaohitimu Elimu ya Msingi katika Shule hii mwaka huu.. 

















Jumanne, 2 Septemba 2014

NAIBU WAZIRI AWAAGIZA MAAFISA ELIMU KUWARUDISHA WANAFUNZI WATORO SHULENI


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Jenista Mhagama amewaagiza Maafisa Elimu wote nchini kuhakikisha wanafunzi walioacha shule kwa sababu mbalimbali wanarudi shuleni ili kuendelea na masomo.

Naibu Waziri alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki  wakati wa ziara yake mkoani Pwani kukagua miradi inayojengwa na Mpango wa Maendeleo  ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Elimu ya Sekondari (MMES). Shule zilizotembelewa ni Nyamisati, Mkamba na WAMA Nakayama zote zikiwa za sekondari na shule ya Msingi ya Mazoezi Vikindu, .

Aliwataka Maafisa Elimu  kufuatilia  sababu za utoro unaojitokeza shuleni na kuandika taarifa juu ya utoro huo na kutafuta njia za kupunguza utoro shuleni. Pia aliwataka Wakaguzi wa Shule wa Kanda pamoja na kazi nzuri wanayoifanya ya kukagua ufundishaji na vigezo, ukaguzi unaofanyika sasa ujikite  katika kujibu hoja ya utoro wa wanafunzi katika shule. Alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Shule kutoka Wizarani Bibi Hidaya Mohamed kutopokea ripoti zisizotoa uelekeo wa namna ya kuwarudisha watoto shuleni.
“Katika kila shule ambapo kutakuwa na utoro mkubwa wa wanafunzi Wakaguzi msipokee ripoti ya ukaguzi isiyotoa majibu kwanini wanafunzi katika shule zetu za msingi na sekondari wanaendelea kutoroka na ripoti ionyeshe hatua zilizochukuliwa kuwarudisha shuleni, mipango na mikakati ya kuhakikisha suala hili halijirudii ili kuwa na ubora wa elimu.” Alisema Mhe. Mhagama   

 Kuhusiana na maslahi ya Walimu Mhe. Mhagama alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga kuanzisha dawati la malalamiko litakalowawezesha walimu  kupeleka malalamiko yao  na kuwataka yafanyiwe kazi haraka iwezekanavyo. Alisema kuanzishwa kwa dawati hilo kutawapunguzia adha walimu ya kupoteza muda kufuatilia madai yao na badala yake watatumia muda huo kuwafundisha wanafunzi.
                                      
“Sitaki walimu hawa tunaowaleta huku wapoteze muda mwingi katika majengo ya Halmashauri kufuatilia madai yao kwani hawa ndio watumishi wengi kwenye Halmashauri hakikisheni mnawatengea dawati maalumu la kushughulikia kero zao.”Alisema Mhe.  Mhagama.