Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya wananchi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi Kwa uadilifu, ubunifu, na weledi wa hali ya juu ili vijana wanamaliza kwenye vyuo hivyo wawe na ujuzi na uwezo wa kujiajiri wenyewe.
Ijumaa, 3 Machi 2017
WAZIRI WA ELIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA DFID.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jana amekutana na kufanya mazungumzo na washirika wa Maendeleo kutoka nchini
Uingereza (DFID) mjini Dodoma ambapo Kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuboresha Miundombinu
katika sekta ya Elimu
Jumatano, 1 Machi 2017
Wizara ya Elimu yahamia Dodoma
Waziri wa Elimu
sayansi na teknolojia profesa Joyce ndalichako leo ametanga za kuwa
wizara hiyo imehamia rasmi Dodoma. Viongozi wakuu wote akiwemo mhe.waziri,
mhe.naibu waziri, katibu mkuu, naibu Makatibu Wakuu wote tayari wamesharipoti
Dodoma katika awamu hii ya kwanza.
Mawasiliano yote
yafanyike kupitia anuani ifuatayo:
Katibu mkuu
Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia
S.L.P. 10
DODOMA
Namba ya simu: 026-
2963633
![]() |
viongozi wa juu wa wizara wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vilivyochini ya wizara hiyo |
![]() |
Waziri wa Elimu profesa joyce ndalichako akitangaza kuhamia rasmi makao makuu ya nchi, Dodoma. |
![]() |
viongozi wa wizara, wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya wizara ya Elimu wakifuatilia maelekezo kutoka Kwa waziri wa Elimu. |
![]() |
Viongozi wa wizara wakikagua majengo ya ofs za wizara ya Elimu. |
Jumatatu, 20 Februari 2017
Serikali za Tanzania na China zatia saini ujenzi wa Chuo cha VETA Kagera
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi na Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na Biashara ya Jamhuri ya watu wa
China nchini Tanzania Lin Zhiyong wametiliana saini makubaliano ya ujenzi wa
Chuo cha Ufundi Stadi VETA kitakachojengwa
Gera mkoani kagera
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarishi akibadilishana hati za
makubaliano (MOU) na Mwakilishi wa Masuala
ya Uchumi na Biashara wa Jamhuri ya watu wa China nchini Tanzania Lin
Zhiyong mara baada ya kutiliana saini.
Alhamisi, 16 Februari 2017
Mkutano wa SDGs4 unaendelea leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini DSM nchini Tanzania
Mawaziri kutoka nchi Kumi
tatu, wawakilishi, mabalozi na wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri
wa elimu katika mkutano wan chi za Ukanda wa Afrika Mashariki wa akuaanisha
changamoto zinazofanana katika mfumo wa
elimu ili kubadilishana uzoefu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
Mkutano huo unatarajiwa kuitimishwa leo jioni.
Mawaziri kutoka nchi Kumi
tatu, wawakilishi, mabalozi na wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya waziri
wa elimu katika mkutano wan chi za Ukanda wa Afrika Mashariki wa akuaanisha
changamoto zinazofanana katika mfumo wa
elimu ili kubadilishana uzoefu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
Mkutano huo unatarajiwa kuitimishwa leo jioni.
MKUTANO WA NCHI 13 ZA UKANDA WA A. MASHARIKI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDFELEO ENDELEVU SDGs4 YA ELIMU 2030
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akifungua mkutano wa nchi
kumi na tatu za ukanda wa Afrika Mashariki kuhusu utekelezaji wa Malengo yaMaendeo
Endelevu SDGs4 ya elimu 2030 ambao unafanyika tarehe 15/02/2017 hadi tarehe 16/02/2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Waziri
wa Elimu amebainisha malengo ya mkutano huo kuainisha changamoto zinazofanana
na kubadilishana uzoefu wa namna wa kukabiliana na changamoto hizo, ambapo kwa
pamoja wanahitaji uwepo kwa elimu
jumuishi yenye usawa bila kujali wanakotoka.
Jumatatu, 6 Februari 2017
Waziri wa Elimu atoa vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika sekta ya Elimu nchini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni Mia Saba na Nne, Mia Sita
Ishirini na Saba Elfu na Mia Nane Hamsini Na Sita (704,627,856/=) kwa
Halmashauri ya kwanza ya Kaliua Kati Ya Halmashauri zote Nchini
zilizoshindanishwa katika utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [
(P4r).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako akikabidhi cheti cha ushindi kwa Halmashauri ya Kaliua iliyopata
ushindi wa kwanza Kati ya Halmashauri zote Nchini zilizoshindanishwa katika
utekelezaji wa Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo [ (P4r).
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)