Jumatano, 1 Machi 2017

Wizara ya Elimu yahamia Dodoma


Waziri wa Elimu  sayansi na teknolojia profesa Joyce ndalichako leo ametanga za  kuwa wizara hiyo imehamia rasmi Dodoma. Viongozi wakuu wote akiwemo mhe.waziri, mhe.naibu waziri, katibu mkuu, naibu Makatibu Wakuu wote tayari wamesharipoti Dodoma katika awamu hii ya kwanza.

Mawasiliano yote yafanyike kupitia anuani ifuatayo:
Katibu mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
S.L.P. 10
DODOMA

Namba ya simu: 026- 2963633
Tovuti: www.moe.go.tz

Barua pepe: info@moe.go.tz

viongozi wa juu wa wizara wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vilivyochini ya wizara hiyo

Waziri wa Elimu profesa joyce ndalichako akitangaza kuhamia rasmi makao makuu ya nchi, Dodoma.

viongozi wa wizara, wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya wizara ya Elimu wakifuatilia maelekezo kutoka Kwa waziri wa Elimu.

Viongozi wa wizara wakikagua majengo ya ofs za wizara ya Elimu.

Maoni 12 :

 1. Maendeleo ni kusonga mbele hata kama kuna wanaobeza ila ili kujenga lazima ubomoe. Ubomoe kwanza ndipo ujenge. HONGERA KWA KUHAMIA DODOMA. ILa sisi watu wa Pwani ni wavivu wa kusafiri nashauri Pamoja na serikali kufanya maamuzi ya kuham ia Dodoma Dar es Salaam ofisi ziendleee kuwepo kwa ajili kutoa baadhi ya huduma ambazo sio lazima mteja kufika WizaraniDodoma. Kwa mfono kaka Wakala wa Usajili wa makampuni Brella wamerahisisha usajil;i wa makampuni kwa njia ya mtandao (Jina la Biashara) . Hata Wizara hii ya Elimu iige mfano huu kwa baadhi ya huduma kuwekwa katika mfumo wa kielektronik ili wateja wapate huma TANZANIA TENDWE MBELE KWA KASI, ARI, UWAZI, UKWELI NA HAPA KAZI TU.

  JibuFuta
 2. Watu wenu wa tehama washughulikie suala la mtandao OTEAS

  JibuFuta
 3. Dar kingebaki kitengo cha kushughulikia wateja

  JibuFuta
 4. Naitwa FESTUS CYPRIAN FUSSI, namba yangu ya kidato cha NNE ni S0117/0021 na ya kidato cha sita no S0117/0515 . Naomba mnisaidie kupata mkopo ili niweze kusoma chuo kikuu kwani toka utoto wangu nilipenda sana kuwa daktari hivyo ikanipelekea kusoma PCB na nimepata DIVISION ONE POINTS EIGHT,

  JibuFuta
 5. Wizara naomba uchunguz ufanyike shule ya secondary moreto watoto 19 wamesimamishwa shule bila sababu ya msingi

  JibuFuta
 6. Waziri naomba pia ushughulikie suala la mafao yangu ya kustaafu Mimi James NKWABI Lupande nimemaliza utumishi wangu chuo cha Ualimu Butimba tangu mwaka 2018 mwezi wa sita sijapata haki zangu kabisa ikiwamo kiinua mgongo Na nusu mshahara naishi KWA kuhangaika sana . nimefanya Juhudi za kusafiri Dodoma , dar es salaam lakini nimekuwa sipati majibu ya kuridhisha zaidi ya kuambiwa faili halionekani , njoo Siku Fulani, taarifa zangu Mara hazipatikani maisha ni Magumu Na nguvu sina kwa sasa .0767868975

  JibuFuta
 7. tunawaomba sana mtembelee vyuo vikuu binafsi ..inawezekana vipi mwanafunzi asome bila kua admited na TCU ..na alichaguliwa na chuo huska mwisho wa safar lazma kuwe na suluisho ...wanafunzi wenye vigezo hata na mikopo hawapati kwasabab TCU inashndwa kuwatambua nakutuma majina yao ingawa wanavigezo ..twa waomba sana mtusaidie ili kabla dirisha la mikopa kufungwa tafadhar

  JibuFuta
 8. samahani naomba wizara mchunguze chuo cha afya muyoge kwani matizo ya udanganyifu ya wizi wa ada na miundombinu mibovu inaleta shida katika masomo kwa wanafunzi

  JibuFuta
 9. Mimi ni mwanafunzi wa chuo cha institute of Accountancy Arusha nalipiwa mkopo ila sio asilimia zote sasa nilipopewa boom kwenda kutoa benki nikapoteza sasa hivi nadaiwa Ada na hostel naombeeni msaada mawasialano 0767828332

  JibuFuta
 10. Mimi ni mwalimu wa sekondari nilituma barua ya kuomba kuhamishiwa chuo cha Ualimu Butimba tarehe 23/03/2016 mpaka leo sijapata mrejesho wa barua hiyo.Naomba ofisi yako ifuatilie barua yangu ili nipate majibu. Kwenye barua hiyo nilionesha elimu yangu (Diploma in Education, Bachelor of Education in policy,planning and Management pamoja na Masters of Educational Planning and Administration). 0756378770/ 0784378770

  JibuFuta
 11. Mimi naitwa Innocent Stephen Rimoy mwanachi wa kawaida naomba niishauri wizara ya elimu juu ya hii changamoto ya mabweni kuchomwa moto kila shule ya bweni au hostel kuwe na sharti la kufunga camera za usalama ndani na nje ya mabweni shule zote ziwe za serikali au binafsi na ziwe na waangalizi matron kwa wasichana na patron kwa wavulana,hizi zitasaidia kudhibiti hivi vitendo kwa asilimia kubwa kwani kuna baadhi ya mwanafunzi wakorofi na usalama wa nje ya majengo hayo na kuokoa kwa kiasi kikubwa roho za hawa watoto wasiokuwa na hatia naomba mlichukue wazo langu maana na mimi ni mzazi.

  JibuFuta