Alhamisi, 26 Juni 2014

TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WAZIRI WA ELIMU

Taarifa za uzushi zilizojitokeza jana katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa amepata ajali na kufariki akiwa safarini kuelekea Mwanza hazifai na zinaleta usumbufu kwa watumishi, familia na jamii kwa ujumla .

Tunaomba watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.

Maoni 3 :

 1. Hivi hawa wanaozusha habari kama hizi wanakuwa na lengo gani hasa. Ila nadhani TCRA sasa inaweza kujua nani ni mwanzilishi wa kuandika habari za uzushi na zisizokuwa na maadili,kwani wanakuja na teknolojia mpya ya kufuatilia mitandao ya kijamii. Pole sana Mh. Waziri

  JibuFuta
 2. Hapo swali la msingi ninalojiuliza ni kuwa: kwa nini muheshimiwa azushiwe swala zito kama hilo???? Mimi hapo nadhani kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia miongoni ni kama chuki binafsi za watu, siasa chafu likiwemo la utendaji mbovu wa mheshimiwa (kuvuruga elimu ya nchi hii ), kwa hiyo ushauri wangu napenda tu kusema kuwa mheshimiwa awe makini tu katika kila atendalo na mambo yatakwenda vema tu...
  Pia kuhusu TCRA, hao mnawatwisha mzigo tu, hayo mambo ya kukamata wahalifu kwenye mitandao kiachieni kitengo cha CYBERCRIME huko polisi na hawa TCRA wabaki na kazi ya kukuza vipaji vya wana sayansi wanaochipukia kama mimi kwa maendeleo ya nchi

  JibuFuta
 3. Wizara ina mpangani na sisi waalimu ambao hatukapangiwa vituo hususani wale wa arts na miaka ya 2011 2012

  JibuFuta