Jumatano, 9 Agosti 2017

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI.



1.0     Serikali inatarajia kuajiri Walimu 92 wa Shahada na 174 wa Stashahada wa masomo ya Fizikia, Hisabati, Kilimo na Biashara kwa Shule za Sekondari na Walimu 2,767 wa Cheti kwa Shule za Msingi.

2.0     Waombaji kwa shule za Sekondari wawe waliohitimu mafunzo ya Ualimu mwaka 2016 au kabla, na wale wa Shule za Msingi wawe waliohitimu mafunzo yao mwaka 2014 au kabla. 

3.0     Sifa za Waombaji:

3.1     Walimu wa Sekondari:
(i)          Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo moja la kufundishia au zaidi au Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo moja la kufundishia au zaidi pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali. Masomo ya kufundishia ni kati ya Fizikia, Hisabati, Kilimo au Biashara.
(ii)        Stashahada ya Ualimu katika masomo yaliyoainishwa kwenye kipengele Na. 2.1 (i) hapo juu.
(iii)      Cheti cha Kidato cha Sita
(iv)       Cheti cha Kidato cha Nne

3.2     Walimu wa Shule za Msingi:
(i)          Astashahada ya Ualimu iliyotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
(ii)        Cheti cha Kidato cha Nne (wenye cheti Kidato cha Sita watapewa kipaumbele).

4.0     Utaratibu wa Kutuma Maombi:
(a)        Maombi yatumwe kupitia Posta kwa njia ya Rejesta (EMS).  Juu ya bahasha iandikwe kwa mkono "Maombi ya Kazi ya Ualimu - Sekondari au Maombi ya Kazi ya Ualimu - Msingi".

(b)        Mwombaji aambatishe nakala za Vyeti vilivyothibitishwa (Certified) na Mwanasheria pamoja na "Transcript".

NB:  Barua za maombi zisiwasilishwe kwa mkono.  Barua zitakazowasilishwa kwa mkono hazitapokelewa.


5.0     Masuala Mengine ya Kuzingatia:
(a)        Mwombaji aandike majina yake yote matatu.  Kama Vyeti vina majina mawili, utaratibu wa kisheria wa kuongeza jina uzingatiwe.
(b)        Mwombaji aambatishe nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.

Mwisho wa kupokelewa maombi ni tarehe 31/08/2017.

Maombi yatumwe kwa:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
             S. L. P. 10,
           40479 DODOMA.           

Imetolewa na:

KATIBU MKUU

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Maoni 3 :

  1. kwahiyo waliomaliza 2015 hawawezi kutuma maombi hayo ya kazi kwa upande wa walimu wa shule za msing?
    mbona walio mzaliza 2014 kurudi nyuma walikuwa wanapewa ajira moja kwa moja? ufafanuzi kidogo hapo plz

    JibuFuta
  2. Tunaomba ufafanuzi zaidi kwa kuwa wanaotuma maombi wengi wao ni wale waliohitimu mwaka 2015 na wale waliohitimu 2016 kwa s/msingi na wanafanya hivyo kwa Kujua kuwa katika Shule za Msingi hakuna wale waliomaliza 2014... Ufafanuzi tafadhali Ahsante

    JibuFuta
  3. HABARI,Ninauridhia kuhusu ajira za walimu wa sekondari ngazi ya diploma katika mchepuo wa masomo ya sanaa, maana naona kama vile tumesaulika kabisa sisi wa sanaa, naomba ufafanuzi kwani hali ni mbaya huku mtaani naomba ninyi serikali mtufikirie na sisi walimu wa masomo ya sanaa kupata ajira

    JibuFuta

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.