Jumatano, 1 Machi 2017

Wizara ya Elimu yahamia Dodoma


Waziri wa Elimu  sayansi na teknolojia profesa Joyce ndalichako leo ametanga za  kuwa wizara hiyo imehamia rasmi Dodoma. Viongozi wakuu wote akiwemo mhe.waziri, mhe.naibu waziri, katibu mkuu, naibu Makatibu Wakuu wote tayari wamesharipoti Dodoma katika awamu hii ya kwanza.

Mawasiliano yote yafanyike kupitia anuani ifuatayo:
Katibu mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
S.L.P. 10
DODOMA

Namba ya simu: 026- 2963633
Tovuti: www.moe.go.tz

Barua pepe: info@moe.go.tz

viongozi wa juu wa wizara wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vilivyochini ya wizara hiyo

Waziri wa Elimu profesa joyce ndalichako akitangaza kuhamia rasmi makao makuu ya nchi, Dodoma.

viongozi wa wizara, wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya wizara ya Elimu wakifuatilia maelekezo kutoka Kwa waziri wa Elimu.

Viongozi wa wizara wakikagua majengo ya ofs za wizara ya Elimu.

Maoni 5 :

 1. Maendeleo ni kusonga mbele hata kama kuna wanaobeza ila ili kujenga lazima ubomoe. Ubomoe kwanza ndipo ujenge. HONGERA KWA KUHAMIA DODOMA. ILa sisi watu wa Pwani ni wavivu wa kusafiri nashauri Pamoja na serikali kufanya maamuzi ya kuham ia Dodoma Dar es Salaam ofisi ziendleee kuwepo kwa ajili kutoa baadhi ya huduma ambazo sio lazima mteja kufika WizaraniDodoma. Kwa mfono kaka Wakala wa Usajili wa makampuni Brella wamerahisisha usajil;i wa makampuni kwa njia ya mtandao (Jina la Biashara) . Hata Wizara hii ya Elimu iige mfano huu kwa baadhi ya huduma kuwekwa katika mfumo wa kielektronik ili wateja wapate huma TANZANIA TENDWE MBELE KWA KASI, ARI, UWAZI, UKWELI NA HAPA KAZI TU.

  JibuFuta
 2. Watu wenu wa tehama washughulikie suala la mtandao OTEAS

  JibuFuta
 3. Dar kingebaki kitengo cha kushughulikia wateja

  JibuFuta
 4. Naitwa FESTUS CYPRIAN FUSSI, namba yangu ya kidato cha NNE ni S0117/0021 na ya kidato cha sita no S0117/0515 . Naomba mnisaidie kupata mkopo ili niweze kusoma chuo kikuu kwani toka utoto wangu nilipenda sana kuwa daktari hivyo ikanipelekea kusoma PCB na nimepata DIVISION ONE POINTS EIGHT,

  JibuFuta