Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce
Ndalichako amezindua Maktaba Mtandao ya Taasidi ya Elimu Tanzania (TET).
Akizindua Maktaba hiyo jijini Dar es salaam Waziri
Ndalichako amesema itasaidia kupunguza changamoto iliyopo ya usambazaji wa
vitabu kwani mara nyingi vimekuwa vikichelewa kufika katika shule kutokana na
ugumu wa miundombinu ya usafirishaji na kuleta usumbufu katika mchakato wa
ujifunzaji na ufundishaji.
Amesema Serikali imeiona changamoto hiyo na kuanzisha
Maktaba Mtandao kama moja ya njia ya
kurahisisha upatikanaji wa machapisho ya Kiada, Ziada, Mitaala Mhtasari,
Kiongozi cha Mwalimu, Miongozo mbalimbali na Moduli za Kufundishia na
kujifunzia kwa wanafunzi walimu na watumiaji wengine.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akizinduz Maktaba Mtandao ya
Taasisi ya Elimu Tanzania katika uzinduzi wa Maktaba hiyo iliyofanyika
jijini Dar es Salaam
“Kumekuwa na lawama katika suala la usambazaji wa vitabu
kwani havifiki kwa wakati, kawaida mwanafunzi anapaswa kukuta vitabu shuleni
lakini hali ilivyo sasa vitabu vinamkuta mwanafunzi shuleni hii si sawa, hivyo
kuwepo kwa Maktaba Mtandao itasaidia katika kupatikana kwa vitabu mapema na
kurahisisha mchakato wa kujifunza" amesisitiza Waziri Ndalichako.
Wakati huo huo Ndalichako ameiagiza Bodi ya Taasisi ya
Elimu Tanzania(TET) kuhakikisha inasimamia uandaaji wa machapisho ya mitaala,
vitabu na machapisho mengine ili yawe na
ubora.
Ameeleza kuwa pamoja na Bodi hiyo kufanya kazi nzuri ya
kusimamia na kuhakikisha vitabu vinavyochapishwa sasa vinakuwa na ubora lakini
bado inapaswa kongeza umakini kwa sababu suala la uandaaji wa vitabu ni endelevu.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiangalia maonesho ya vitabu
vinavyoandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maktaba Mtandao jijini Dar es Salaam
Ndalichako amesisitiza kuwa TET ni moyo wa Elimu nchini kwa kuwa ndio inaandaa mitaala, vitabu, miongozo ya shule za msingi na sekondari pamoja na machapisho mbalimbali ya Elimu, hivyo kukiwa na kasoro katika mchapisho hayo watoto wa Kitanzania watakuwa wamefundishwa vitu ambavyo si sahihi na serikali haitavumilia hilo.
Awali Mkurgenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Aneth
Komba alimweleza Waziri wa Elimu kuwa lengo la kuanzishwa maktaba mtandao hiyo
kurahisisha usambazaji wa machapisho ya Taasisi hiyo katika shule za Serikali,
Binafsi na kwa wadau wengine wa Elimu
Dkt Komba amesema
Maktaba Mtandao iliyozinduliwa inajumuisha vitabu mbalimbali vya kiada
kuanzia ngazi ya Elimu ya awali, msingi na sekondari (kidato cha kwanza mpaka
sita) vinavyochapishwa na taasisi hiyo.
Pia vitakuwepo vitabu vya ziada kutoka
Tanzania na Nchi nyingine.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akicheza na kufurahi na
wanafunzi wa shule ya Fountain Gate wakati wa uzinduzi wa Maktaba Mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania
katika uzinduzi wa Maktaba hiy iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Tunavipataje hivyo vitabu vya mtandaoni kwa wale wenye watoto ambao wako kijijini na hakuna huduma zinazoweza kupata vitabu hivi kama vile...internet,umeme,computer nk? Au huduma hii imelega kusaidia watoto wenu walio na uwezo wa kupata miundombinu hiyo? Je mtoto wa mwananchi myonge mnamsaidiaje ili aweze hata kwenda mjini na kuprint vitabu hivi ili ajisomee??
JibuFutaNashauri kipindi hiki serikari ingegaramia kumpa kila mtoto vitabu vya masomo ili ajisomee hasa watoto ambao hawana computer nyumbani ili wajisomee hya ya mtandao yatanufaisha wachache tu.
JibuFutaKuwa na kipindi maalum kwenye redio ya taifa TBC
JibuFutaTunaomba link ya kuvipata hivyo vitabu vya watoto wa shule za msingi.
JibuFuta