Jumanne, 5 Mei 2015

AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA KKK - CHUO KIKUU CHA DODOMA

Awamu ya pili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Msingi wanaofundisha darasa la I na II yakiendelea katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambapo walimu wengine zaidi ya elfu nne wameshiriki kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Kagera, Katavi, Geita na Mwanza

 Katika awamu ya kwanza mikoa iliyoshiriki ni pamoja na Arusha, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Rukwa, Ruvuma, Tanga na Singida.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni