Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wakala wa majengo nchini TBA
kulipa madeni wanayodaiwa na Wananchi mbalimbali kufuatia ujenzi unaoendelea wa
Shule ya Sekondari wavulana Ihungo iliyopo Wilayani bukoba mkoani kagera.
Waziri Ndalichako amesema kuwa tayari
wizara imekwisha ilipa TBA zaidi ya bilioni Tisa na garama ya ujenzi kwa
mradi wote ni shilingi bilioni 10 nukta 48.
" Mnyonge mnyongeni haki yake
mpeni, nipende kuwapongeza Wakala wa Majengo TBA kwa kazi nzuri ambayo
wameifanya.
"Lakini nasikikitika sana
kupokea malalamiko kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa inayoeleza kuwa bado kuna
Wananchi wanaidai TBA kutokana na kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile
mbao, matofali, na vibarua ambao wameshiriki katika ujenzi huo wa shule ya
wavulana Ihungo na kuwa mpaka sasa hawajalipwa, hii haipendezi ni vyema TBA
kuhakikisha inalipa madeni hayo,"alisema Waziri Ndalichako.
Waziri Ndalichako amesema haoni
sababu kwa nini wananchi hawajalipwa wakati tayari Serikali imekwisha ilipa
TBA, ni vyema wakalipwa ili kusaidia kuepusha migogiro isiyo ya lazima baina ya
Serikali na wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa TBA mkoa
wa Kagera Salum Chanzi amekiri kuwepo kwa sababu mbalimbali zilipelekea
mradi kutokamilika kwa wakati na hivyo kuomba wapewe muda zaidi mpaka mwezi
machi mwaka huu ili waweze kukamilisha.
"Mheshimiwa Waziri mradi huu
haijakamilika kwa wakati uliokuwa umepangwa kutokana na changamoto ya kuagiza
vifaa kutoka nje ya mji wa bukoba, na hii inatokana na bei wakati mwingine kuwa
kubwa hapa bukoka lakini nje ya hapa tunavipata kwa bro nafuu,"
alisema Chanzi.
Chanzi amemhakikishia Waziri Ndalichako kuwa tayari madeni yote
wanayodaiwa na wananchi katika ujenzi huo wa Ihungo Sekondari yamewasilishwa
kwenye Taasisi yake yanafanyiwa kazi na wahusika wote watalipwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.