Jumanne, 12 Aprili 2016

Profesa Ndalichako: Wekeni malengo katika utendaji kazi


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia  na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kujiwekea malengo katika utendaji kazi wao ili waweze kutimiza malengo makubwa ya sekta ya elimu.


Profesa Ndalichako aliyasema hayo wakati  akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kutoka Makao Makuu katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee ikiwa ni mara ya kwanza kukutana nao tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi lengo likiwa ni kuwasikiliza lakini pia kujadiliana nao namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara hiyo.

Waziri Ndalichako aliwataka wafanyakazi kufanya kazi  kujituma, kutoa huduma bora kwa wakati kwa kuwa  ni watumishi wa umma na maana ya mtumishi wa umma ni kuwa na  wajibu wa kuwatumikia wananchi ili wapate haki yao kwa wakati kwani haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyoptea.

Amewataka watumishi hao kuipende kazi yao,  kwa maana mtumishi anayependa kazi yake  uifahamu kwa undani wake na inakuwa rahisi kuwatyumika wananchi bila ya kuwa na wasiwasi na kujiamini zaidi

 “kila mfanyakazi ni lazima kujivika joho la Wizara kwa maana ya kuijua Wizara vizuri, misingi yake, dira pamoja na sera zinazotuongoza katika utendaji kazi wetu ili tuweze kufikia malengo ya kuinua ubora wa elimu” alisisitza Ndalichako.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi Omary Mkali alimshukuru Waziri kwa kukutana na watumishi na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri ili kuweze kufikia lengo kwa pamoja la kuinua ubora wa Elimu nchini.


1   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiingia katika ukumbi wa Karimjee kuongea na wafanyakazi wa Wizara.


1      Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Maimuna Tarishi akimkaribisha Waziri wa Elimu kuongea na wafanyakazi.


1   waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wafanyakazi wa Wizara.



1     wafanyakazi wa Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi wakimsikiliza Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.



Alhamisi, 7 Aprili 2016

TAARIFA KWA UMAA


YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
 

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.

Taarifa hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare  watakazo vaa wakati wa kazi.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

 

IMETOLEWA NA

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

07/04/2016

Jumanne, 5 Aprili 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi atembelewa na Mabalozi wa Ireland na Finland Ofisini kwake

 
 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akiongea na Balazoi wa Ireland Bi Fionnuala Gilsenan aliyefika ofisini kwake leo asubuhi kwa ajili ya kujadili miradi mbalimbali ya elimu inayoendeshwa nchini.





 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akiongea na Balazoi wa Finland Bw. Pelleka Hakka aliyefika ofisini kwake leo asubuhi kwa ajili ya kujadili miradi mbalimbali ya elim inayoendeshwa nchini pamoja nao ni Oskar Kass na Mkurugenzi wa Kitengo cha Uratibu wa masuala ya elimu Kikanda na Kimataifa 
 
 
 
 
 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi afanya ziara shule za Msingi za Diamond na Olympio



Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Eng Stella Manyanya akipokelewa na viongozi wa shule za Msingi Diamond na Olympio wakati wa ziara yake.





Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Eng Stella Manyanya akitembelea mazingira ya shule ya Msingi Olympio



Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Eng Stella Manyanya akiongea na wanafunzi wa  shule ya Msingi Olympio




Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Eng Stella Manyanya akiwa darasani na wanafunzi.



Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhe. Eng Stella Manyanya akizungumza na walimu wa shule za Msingi Olympio na Diamond