Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kujiwekea malengo katika utendaji
kazi wao ili waweze kutimiza malengo makubwa ya sekta ya elimu.
Profesa
Ndalichako aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kutoka
Makao Makuu katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee ikiwa ni mara ya kwanza
kukutana nao tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na
Ufundi lengo likiwa ni kuwasikiliza lakini pia kujadiliana nao namna bora zaidi
ya kuboresha utendaji kazi katika wizara hiyo.
Waziri
Ndalichako aliwataka wafanyakazi kufanya kazi kujituma, kutoa huduma bora kwa wakati kwa
kuwa ni watumishi wa umma na maana ya mtumishi
wa umma ni kuwa na wajibu wa kuwatumikia
wananchi ili wapate haki yao kwa wakati kwani haki iliyocheleweshwa ni sawa na
haki iliyoptea.
Amewataka
watumishi hao kuipende kazi yao, kwa
maana mtumishi anayependa kazi yake uifahamu
kwa undani wake na inakuwa rahisi kuwatyumika wananchi bila ya kuwa na wasiwasi
na kujiamini zaidi
“kila mfanyakazi ni lazima kujivika joho la
Wizara kwa maana ya kuijua Wizara vizuri, misingi yake, dira pamoja na sera
zinazotuongoza katika utendaji kazi wetu ili tuweze kufikia malengo ya kuinua
ubora wa elimu” alisisitza Ndalichako.
Akizungumza
kwa niaba ya watumishi Omary Mkali alimshukuru Waziri kwa kukutana na watumishi
na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri ili kuweze
kufikia lengo kwa pamoja la kuinua ubora wa Elimu nchini.
1 Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiingia katika ukumbi wa Karimjee kuongea na
wafanyakazi wa Wizara.
1 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Maimuna Tarishi akimkaribisha Waziri wa Elimu kuongea na
wafanyakazi.
1 waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiongea na wafanyakazi wa Wizara.
1 wafanyakazi wa Wizara ya Elimu Sayansi
Teknolojia na Ufundi wakimsikiliza Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.