Walimu wanaofundisha
darasa la awali hadi la tatu katika shule ya msingi Nyerere, Mughanga na shule
ya wanafunzi wenye mahitaji Maalumu Ikungi zote zilizopo mkoani Singida
wameeleza kuwa mbinu za kuimba, kucheza, kujifunza kwa kushirikisha
wanafunzi zinawasaidia wanafunzi kuelewa kwa haraka pamoja na kuwa na umahiri
wa kusoma na kuandika na kuhesabu.
Akizungumza na timu ya
wanahabari walio katika ziara ya kufuatilia hali ya ufundishaji na ujifunzaji
wa KKK na kuangalia hali ya uboreshaji wa miundombinu mkoani humo Mwalimu
Salome Kyomo amepongeza jitihada za serikali za kuwapatia walimu mafunzo ya KKK
kwa kuwa mbinu na zana za kufundishia zimeboreshwa.
Kwa upande wake
mratibu wa taaluma wa shule ya msingi Nyerere Lisu Mnyambi amesema shule
hiyo ilipokea kiasi cha shilingi Milioni 192 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kupitia Programu ya Lipa kulingana na matokeo. ambazo zimetumika
kujenga vyumba vya madarasa 8, ujenzi wa matundu ya vyoo na hivyo kupunguza
msongamano wa wanafunzi madarasani.
Walimu wa shule ya
Msingi Mughanga mkoani Singida wakiwa kwenye moja ya darasa la Pili
ambalo mbinu mbalimbali za kujifunzia na kufundishia , (KKK) zipo katika darasa
hilo.
Baadhi ya vyumba vya
madarasa katika shule ya msingi Nyerere iliyopo mkoani Singida ambayo imejengwa
na fedha zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia
Program ya lipa kulingana na Matokeo, (P4R)
Mwanafunzi wa darasa
la Pili katika Shule ya Endeberg iliyopo Manyara vijijini akisoma kile
kilichoandaliwa na Mwalimu wake huku wanafunzi wengine wakimsikiliza. Lengo la
Mwalimu hapo ni kujua wanafunzi wake wanaelewa kile alichowafundisha.
I love to learn.
JibuFuta