Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo amewataka
watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi katika kutekeleza majukumu
yao ya kila siku.
Dk.
Akwilapo ameyasema hayo wakati wa kikao cha kwanza cha watumishi wa wizara hiyo
kilichofanyika mkoani Dodoma tangu serikali itangaze rasmi kuhamishia makao
makuu ya nchi mkoani humo.
Dk.
Akwilapo amesema utii, ushirikiano,bidii na upendo mahali pa kazi miongoni mwa
watumishi ndiyo silaha pekee ya kufikia malengo ambayo Wizara imejiwekea katika
kuinua Sekta ya Elimu hapa nchini.
"Nipende
kuwapongeza watumishi wote kwa kushiriki majukumu mbalimbali ya Wizara ikiwemo
kuisimamia vyema miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara, nawasihi sana
tuusifanye kazi kwa kujitenga, ushirikiano miongoni mwetu ni jambo la msingi
sana na tukiwa na Umoja basi mafanikio lazima yatapatika katika Sekta hii ya
Elimu,"alisema Dk.Akwilapo.
Pia
Katibu Mkuu Dk.Akwilapo amewataka watumishi kuwa na matumizi sahihi ya
Teknolojia,kujibu barua mbalimbali kwa wakati pamoja na kushughulikia faili
zinazofika kwenye ofisi zao ndani siku mbili
na siyo kuziacha zikae muda mrefu.
Kupitia
kikao hicho watumishi pia walipata fursa ya kuwaaga viongozi ambao walitumikia
Wizara hiyo ambao hivi sasa wamehamiahiwa Wizara nyingine na kuwakaribisha
viongozi wapya ambao wamehamia kwenye Wizara hiyo.
Viongozi
waliokaribishwa ni pamoja na Naibu Waziri William Ole Nasha na Naibu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe na walioagwa ni Naibu Waziri
Mhandisi Stella Manyanya na Profesa Saimon Msanjila ambaye hivi sasa ni Katibu
Mkuu anayesimamia Sekta ya Madini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.