Serikali ya Korea leo imeikabidhi msaada wa dawa zenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Moja kwa
Serikali ya Tanzania ikiwa ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya nchi hizo
mbili.
Msaada huo umekabidhiwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako jijini
Dar es Salaam ili zitumike katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba
Muhimbili (MUHAS) Kampasi ya Mloganzila.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa pamoja na Wajumbe
wa Kamati za Bunge la Jamhuri ya Watu wa Korea wakisalimiana na Wagonjwa katika Hospitali ya Taaluma na
Tiba ya Mlongazila jijini Dar es Salaam mara baada ya Korea kutoa msaada wa kwa ajili ya Hospitali hiyo.
Mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Ndalichako ameishukuru
Serikali ya Korea kwa msaada huo na kuwataka wanafunzi wanaosoma katika chuo
hicho kutumia vema miundombinu ya Chuo kwa
kujifunzia na kufundishia ili kujijenga kitaaluma kwalengo la kumaliza tatizo la uhaba wa Madaktari na Wataalam
wa Afya hapa nchini.
Kiongozi
wa Ujumbe wa Kamati za Bunge la Jamhuri
ya Watu wa Korea Jun Hey Sook
akimkabidhi rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako msaada wa dawa uliotolewa na
nchi hiyo kwa ajili ya Chuo cha Taaluma na Tiba cha MLOGANZILA kilichopo jijini
Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano ya dawa hizo
Kiongozi wa Ujumbe wa Korea wa Kamati ya
Afya na Huduma za Jamii ya Bunge la nchi hiyo, Jun Hey Sook amesema msaada huo
wa dawa ni ushirikiano katika kuboresha sekta ya Afya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.