Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka Wanawake
nchini kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuonyesha Thamani ya Mwanamke
katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Waziri Ndalichako amesema bidii pekee katika
shughuli mbalimbali za kujiletea Maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa
ujumla ndiyo itaonyesha mchango wa Mwanamke na kumfanya athaminiwe na
kumuwezesha kupata nafasi kubwa na nzuri zaidi za kutumikia Taifa ikiwa ni
pamoja na kufuta dhana potofu ya kuwa Mwanamke hawezi.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya Wajumbe wa Jukwaa la Akademia katika kuadhimisha siku ya Wanawake
Duniani shughuli ambayo imefanyika
jijini Dar es salaam.
Waziri
Ndalichako amesema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani
yaliyoandaliwa na Taasisi ya Akademia ya
Sayansi Tanzania walati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ili kujadili
mchango wa Mwanamke katika kuleta Maendeleo Endelevu ambalo limeshirikisha
Wanawake na Wadau wengine kutoka nchi mbalimbali.
Kwa
upande wake Spika Mstaafu Anne Makinda amesema wanawake wanapaswa kuhakikisha
wanapata Elimu ambayo itawawezesha kujikwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwa
na uthubutu wa kufanya shughuli ambazo wanaamini watazifanya kwa umakini ili
kuonyesha uwezo walionao katika jamii inayowazunguka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.