- AKIRI KUWA SASA SHULE ZIMEKUWA MPYA
Zaidi ya shilingi bilioni 2
zimetumika kujenga na kukarabati miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari
katika Mkoa wa Lindi na hivyo kuchochea kuongeza kwa kiwango cha ufaulu
miongoni mwa wanafunzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Lindi Godfrey Zambi wakati akizungumza na timu ya wanahabari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari ameeleza kuwa Mpango huo Maalumu wa Lipa Kulingana na
Matokeo yaani EP4R umebadilisha muonekano wa mazingira na kuzifanya shule
nyingi za Mkoa huo kuwa mpya.
Muonekano wa moja ya Jengo
la darasa la Shule ya Msingi Kitomanga lililopo katika Halmashauri ya Lindi
Vijijini Mkoani Lindi liliojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia
Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
Zambi amesema kupitia EP4R Mkoa
huo umejenga vyumba vya madarasa 30 kwa shule za Msingi, vyumba 22 kwa shule za
sekondari, maabara 6 zimekarabatiwa, na ujenzi wa matundu ya vyoo 84 na kuwa
ujenzi na michiro ya miundombinu hiyo imekuwa ikizigatia mahitaji ya wanafunzi
wenye ulemavu.
Hata hivyo ameeleza kuwa bado
ujenzi wa miundombinu mingine unaendelea katika shule za Msingi na Sekondari
ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika shule
mbalimbali.
“Kabla ya ukarabati nikiri kuwa
hali ilikuwa siyo nzuri katika miundombinu ya shule lakini kupitia EP4R Mkoa wa
Lindi miundombinu yake imebadilika sana ambapo pia imeongeza hamasa ya
wanafunzi kusoma na hivyo kuongeza ufaulu, pia utoro umepungua sana maana
kuboreka kwa miundombinu kumehamasisha wanafunzi kupenda shule,” anasema Zambi.
1. Muonekano wa moja ya Jengo la darasa la
Shule ya Sekondari Kilwa lililopo katika Halmashauri ya Lindi Mkoani Lindi
liliojengwa na Wizara ya Elimu, Saynsi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa
Kulingana na Matokeo (EP4R).
Mkuu huyo wa mMkoa amesema kuwa
ukarabati wa maabara kwa Mkoa huo pia umesaidia sana mwitikio wa wanafunzi
wanaosoma masomo ya sayansi kwa kuwa hivi sasa wanafanya mazoezi kwa vitendo na
hivyo kuwafanya waelewe kwa urahisi.
Mkuu huyo wa mkoa amekiri kuwa
bado mwitikio wa Elimu katika Mkoa huo uko chini na hivyo kuwafanya
watoto walio wengi kutothamini Elimu.
“Mwitikio wa wananchi kuhusu
Elimu bado uko chini, na wazazi ndiyo wanaochangia kwa kuwa ndiyo wanaowapeleka
watoto wao kwenda kufanya shughuli za shambani ikiwemo kutuma korosho pamoja na
kushiriki katika masuala ya mila na tamaduni za kuwapeleka watoto kwenye
unyago,” anasema Zambi.
Muonekano wa moja ya Jengo la darasa la
Shule ya Msingi Masoko lililopo katika Halmashauri ya Kilwa Mkoani Lindi liliojengwa
na Wizara ya Elimu, Saynsi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa Kulingana na
Matokeo (EP4R).
Mkuu huyo amesisitiza kuwa ni
vyema wazazi wakatambua umuhimu wa Elimu ili kuwasaidia watoto kupenda shule
kwa lengo la kuliletea taifa Maendeleo.
Timu ya waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali pamoja na Maafisa kutoka Kitengo Cha Mawasiliano Cha
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wako Mkoani Lindi kwa ajili ya
kufuatilia uboreshaji wa miundombinu inayojengwa na kukarabatiwa na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo,
EP4R.
Mikoa mingine ambayo timu hiyo
itafanya ufuatiliaji ni pamoja na Mkoa wa Mtwara na Songea.
1. Muonekano wa jingo la Choo kilichojengwa
katika Shule ya Msingi Kitomanga iliyopo Wilayani Lindi Vijijini Mkoani Lindi,
Ujenzi choo hicho umetekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia kupitia
Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.