Wakuu wa shule za Sekondari
mkoani Lindi wamesema kuwa ujenzi wa mabweni unaotekelezwa na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa Lipa Kulingana na matokeo, yaani EP4R
katika mkoa huo utasaidia sana kuondoa changamoto ya wananfunzi wa kike kupata
mimba wakiwa katika umri mdogo.
Wakizungumza na wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali Mkuu wa shule ya sekondari ya Ruangwa Mwalimu Herber
Ngonyani amesema kupitia mradi wa EP4R shule hiyo imeweza kujenga mabweni
Mawili ambayo yanauwezo wa kuchukua wanafunzi Laki moja na sitini kwa wakati
mmoja, huku Mkuu wa shule ya Sekondari Nkowe Ahmed Maliki akikiri kuwa shule
yake imejenga mabweni mawili yenye uwezo
wa kuchukua wanafunzi mia moja na ishirini na nane kwa mara moja.
Muonekano wa
bweni katika Shule ya Sekondari Ruangwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi. Bweni
hilo limejengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya
Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R).
Wakuu hao wa shule wameeleza
kwa muda mrefu watoto wa kike katika wilaya hiyo wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto ya kutembea umbali mrefu na hivyo kukumbana na vishawishi ambavyo
hupoteza ndoto za wanafunzi hao.
“ Nikiri kuwa mwamako wa
Elimu katika Wilaya yetu bado uko chini hivyo hata hamasa ya wazazi na watoto
nayo iko chini katika suala zima la Elimu, sasa hiki ambacho Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia inachokitekeleza
kupitia mradi wa Lipa kulingana na matokeo kwa kweli ni mkombozi kwa watoto wa
kike kwa kuwa sasa watasoma kwa utulivu tena wakiwa katika mazingira ya shule
kutokana na ujenzi huu wa mabweni,”anasema Mwalimu Herbert Ngonyani.
Kwa upande wake Mkuu wa
shule ya Sekondari ya Nkowe Ahmed Maliki amessitiza kuwa uwepo wa mabweni
utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya utoro miongoni mwa wanafunzi
pamoja na kuwasidia wanafunzi wa kike kupuka mazingira hatarishi ya kutembea
umbali mrefu takribani kilometa 4 hadi tano kwa siku kwa ajili ya kufika
shuleni.
Muonekano wa
bweni katika Shule ya Sekondari Nkowe Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi. Bweni hilo
limejengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Programu ya Lipa
Kulingana na Matokeo (EP4R). Bweni hilo litasaidia kuondoa changamoto ya
wanafunzi wa kike kupata mimba katika umri mdogo.
Mwalimu Malik amesema kuwa
mabweni hayo yatasaidia siyo tu kuhuduia wanafunzi wa wanaotoka kwenye mkoa wa
Lindi pekee bali wananfunzi kutoka mikoa mbalimbali watanufaika na mabweni
hayo.
Katika kutekeleza uboreshaji
wa Miundombinu ya shule za msingi, moja ya shule ambazo zilipatiwa fedha za
kujenga miundombinu hiyo ni pamoja na shule ya msingi Nangumbu ambayo ilipatiwa
kiais cha shilingi Milioni sitini na sita kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa vitatu na matundu ya vyoo sita lakini shule hiyo imeweza kujenga
vyumba vya madarasa vinne, ofisi moja na matundu kumi ya vyoo.
Timu ya wananhabari ambayo
imeambatana na maafisa wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknolojia kesho itaendelea na ziara yake Mkoani Mtwara ikiwa na lengo la
kuangalia hali ya uboreshaji wa miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari
inayotekelezwa kupitia program ya lipa kulingana na matokeo.
Muonekano wa
moja ya darasa liliojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia
Programu ya Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) katika Shule ya Sekondari Nkowe
iliyopo katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.