Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Norway nchini Tanzania Elisabeth Jacobsen mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo
mengine wamezungumzia kuendeleza ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya nchi
hizo mbili.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akifanya mazungumzo na Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen kuhusu Sekta ya Elimu.
Waziri Ndalichako ameishukuru
serikali ya Norway kwa kuendelea kufadhili sekta ya elimu kupitia Mfuko wa Global Partnership for Education (GPE ) na amemuhakikishia Balozi Jacobsen kuwa
fedha zote zinazotolewa na kupitia mpango huo zitatumika kama ilivyokusudiwa.
Waziri Ndalichako amevitaja vipaumbele vya ufadhili
huo kuwa ni masuala ya uthibiti ubora wa shule, ununuzi wa vitabu na kutoa mafunzo kwa walimu walio kazini.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen pamoja na viongozi wengine Mjini Dodoma
Kwa upande wake Balozi wa
Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, ameipongeza Serikali ya Tanzania
kwa kupiga hatua kubwa katika elimu na kueleza kuwa wanaridhishwa na utekelezaji
wa mradi wa uanzishaji Kituo cha kufuatilia Hewa ya Ukaa katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiagana na Balozi wa Norway Elisabeth Jacobsen
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.