Jumatano, 7 Septemba 2016

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia afungua Kikao cha Maandalizi ya Makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya jamii

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi akifungua kikao cha maandalizi ya makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga

Ofisa wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, akisoma historia fupi ya vyuo vya maendeleo ya jamii wakati wa kikao cha maandalizi ya makabidhiano ya vyuo hivyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


Katibu Mkuu wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarishi kwenye kikao cha maandalizi ya makabidhiano ya Vyuo vya Maendeleo ya Jamii. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni