Alhamisi, 8 Septemba 2016

Kaimu Kamisha Afungua Maadhimisho ya Siku ya Kisoma Duniani



Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholaus  Bureta akifungua   maadhimisho  ya siku ya Kisomo Duniani (International Literacy Day)Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maimuna Tarish, katika ukumbi wa makumbusho ya Taifa. Maadhimisho haya yalienda sambamba na ufunguzi wa ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu.
 



Mwakilishi wa UNESCO nchini Bi.Zulmira Rodriguez akimkabidhi Kaimu kamishna wa Elimu ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu wakati wa maadhimisho ya siku ya kisomo duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 




Kaimu Kamishna wa Elimu Nicholaus Bureta akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa  wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, mashirika ya Kimataifa ya maendeleo pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali wakionyesha ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu mara baada ya uzinduzi wake rasmi. Kushoto mwanzoni ni Mwakilishi wa UNESCO nchini Bi.Zulmira Rodriguez.


Kaimu Kamishna wa Elimu Nicholaus Bureta akiwakabidhi ripoti ya Kimataifa ya Ufuatiliaji wa Elimu baadhi ya walimu wakuu wa shule za Msingi nchini mara baada ya uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya kisomo duniani yaliyofanyika  katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.