Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Saimon Msanjila
amezindua mkutano wa 24 wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ulioanza leo katika
ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine mjini Morogoro ambapo amewaasa
watumishi kufanya kazi kwa weledi na maarifa zaidi ili kuleta ufanisi
utakaokuwa na tija.
Profesa
Msanjila amesema ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu ni lazima
watumishi kubadilika na kufanya kazi kwa kujituma na kuachana na tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea.
Profesa
Msanjila amesisitiza kuwa wizara ina wajibu wa kuhakikisha nchi inakuwa
na elimu bora ili kupata wahitimu na wataalam watakaowezesha nchi kufikia lengo
la kuwa na uchumi wa viwanja.
Aidha,
amewataka wajumbe wa mkutano kujielekeza zaidi katika mbinu na mikakati ya
utekelezaji kwa kushirikiana na uongozi wa Wizara ili kukamilisha malengo ya
mwaka 2016/17 na malengo mapya ya mwaka 2017/18.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.