Jumanne, 23 Mei 2017

Ushiriki wa Waziri wa Elimu Sayansi, na Teknolojia katika Mkutano Mkuu wa 18 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliifanyika hivi karibuni Ikulu jijini Dar Es Salam, Tanzania.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakibadilishana uzoefu na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Kawaida  wa Wakuu wa Nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika mwishoni mwa wiki Ikulu, jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania. Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki likiwa katika picha ya pamoja na viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 18 uliofanyika hivi karibuni Ikulu jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa na baadhi ya Mawaziri wa Tanzania wanaounda Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo uliofanyika hivi karibuni, Ikulu jijini Dar es Salaam, Tanzania

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni