Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya ameonyesha
kutokuridhishwa na hatua ya Halmashauri ya Kinondoni kuhamisha fedha za ujenzi
wa madarasa, mabweni na vyoo zilizokuwa zimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi
na Teknlojia kupitia mradi wa lipa kwa matokeo kwa shule ya Sekondari ya
Kambwangwa na kupelekwa katika Shule ya sekondari Mbweni tete bila kufuata
utaratibu wa kuitaarifu wizara iliyotoa fedha hizo.
Mhandisi
Manyanya ameyaeleza hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya
kuzitembelea shule mbalimbali kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ujenzi na
ukarabati unaofanywa na Mradi wa Lipa kwa Matokeo (P4R). Amesema kuhamishwa kwa
mradi si tatizo lakini kuhamisha bila kutoa taarifa ndo tatizo lilipo kwani
wizara imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi huo hivyo ni lazima kufanya
ufatiliaji ili kuweza kujirizisha kama ujenzi unafanyika lakini wakati
najiandaa kwenda Kambagwa ndipo alipotaarifa kuhusu kuhamishwa kwa mradi huo.
“Leo
wakati tunataka kuanza kwenda kuangalia ujenzi ulipofikia lakini tukapewa
taarifa kuwa mradi huo haupo Kambangwa na ulihamishwa kupelekwa eneo jingine,
hivyo ni muhimu kupeana taarifa maana kuhamishwa kwa mradi kunaleta hoja za
ukaguzi” alisisitiza Mhandisi Manyanya.
Naibu
Waziri amesema ujenzi wa miundombinu hiyo katika Halmashauri mbali mbali
imekuja baada ya wizara ya Elimu kwa kushirikiana na TAMISEMI uwepo wa umuhimu
wa kuongeza miundombinu ya madarasa,
mabweni na vyoo katika baadhi ya shule ili kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahili kwa ajili ya kujiunga na masomo ya
kidato cha tano. Amesma lengo la serikali ni kuona wanafunzi wote waliofaulu
wanapata nafasi ya kuendelea na masomo yao ya kidato cha tano bila mmoja
kuachwa.
Shule nyingi zimezidiwa na idadi ya wanafunzi.
JibuFutaLengo liwe kuongeza miundo mbinu bila kuvunja sheria na taratibu tulizojiwekea ili wanafunzi wa Shule za Msingi wasizidi 45 kwenye chumba 01 cha darasa, sekondari kidato cha I-IV wasizidi 40 na kidato cha V-VI wasizidi 30. Tukifanya hivyo tutakuwa sawa.
Ukubwa wa shule kulingana na usajili uzingatiwe katika kila shule hasa wakati wa mgawo wa wanafunzi wa Kidato cha Kwana na cha Tano. Shule zisipelekewe wanafunzi kama Tahasusi husika haikusajiliwa katika shule hiyo.