Kaimu Mkurugenzi mafunzo ya Ualimu Basiliana Mrimi amezindua mradi wa shilingi milioni 500 utakaosaidia kuimarisha Ufundishaji na ujifunzaji kwenye Chuo cha Ualimu, Patandi kilichopo mkoani Arusha.
Akizundua
Mradi huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Mrimi amesema mradi huo utasaidia Kupima
macho watoto wa shule za msingi na kuwapatia vifaa wanafunzi wenye uoni hafifu,
Kutoa mafunzo kazini kwa wakufunzi 12 na walimu 4 wa shule za msingi zilizopo
kwenye mradi.
Pia
mradi huo utasaidia Kusomesha mkufunzi 1 kwa ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD),
Kusomesha wakufunzi 4 kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters) na kuwa mradi
huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Norway.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.