Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka wanafunzi
kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kupata taarifa zitakazowasaidia
kutekeleza fursa mbalimbali za kujiletea Maendeleo.
Waziri
Ndalichako ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Twende kazi na Balozi
mwanafunzi unaohusu ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 23 wa shahada ya
kwanza ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kusisitiza kuwa taasisi nyingine
ziige mfano huo wa Barclays wa kufadhili wanafunzi.
Pia
Barclays imewasaidia vijana 32 Kati ya 200 kuwatafutia ofisi ili kufanya kazi
kwa vitendo kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kuwa tayari kwa kazi.
Uzinduzi
huo pia umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Profesa Sylivia Temu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.