Akizungumza
Mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo Waziri Ndalichako
amesema suala la nchi kuwa na shule au vyumba vya madarasa vya nyasi
litabaki kuwa historia kwa kuwa serikali ya awamu ya Tano inahitaji wanafunzi
wapate Elimu bora inayoenda sambamba na uboreshaji wa miundombinu na hicho ndicho
kinachofanyika hivi sasa.
Akizindua
bweni moja la wasichana katika shule ya Sekondari Semkiwa waziri Ndalichako
ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kununulia vitanda
na magodoro ili bweni hilo lianze kutumika mara moja.
Pia
amewataka watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa namna anavyojitoa katika
kuwatumikia Wananchi wanyonge kwa lengo la kuliletea Taifa Maendeleo.
Ujenzi
wa vyumba hivyo vya madarasa,na vyoo umetekelezwa na Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wa Lipa kulingana na matokeo, (EP4R).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.