Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Elimu ya Ufundi ndiyo nguzo muhimu
ya kufikia ajenda ya serikali ya kuwa Tanzania ya viwanda na kufikia uchumi wa
kati ifikapo 2025.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati
akifungua kongamano la kimataifa la wadau wa Elimu ya Ufundi na mafunzo jijini
Dar es salaam, na kusisitiza kuwa dira ya Maendeleo ya 2025 imeipa Elimu
kipaumbele cha juu kwa kuwa ndiyo kitovu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi
katika jamii.
Makamu wa Rais amesema kuwa
serikali kipitia baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi litaendelea kusimamia na
kuratibu utoaji wa mafunzo katika taasisi za Elimu ya Ufundi ili Taifa liwe na
wataalamu wa kutosha na wenye weledi katika fani mbalimbali kwa Maendeleo ya
Taifa.
Viongozi wengine walioshiriki
mkutano huo wa siku tatu ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa. Joyce Ndalichako, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Avemaria Semakafu, Wakuu wa
Taasisi na wadau mbalimbali.
Kauli mbiu katika mkutano huo ni
Wekeza katika Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Tanzania kuwa ya uchumi wa
viwanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.