Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amesema
zaidi ya watoto milioni mia mbili duniani hawafikii malengo kutokana na umasikini na utapiamlo wanaoupata wakiwa katika umri
mdogo.
Dkt. Semakafu ameyasema hayo wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa pili wa kimataifa wa kujadili maendeleo ya makuzi ya
watoto na kusisitiza kuwa kupitia mkutano huo wadau wataweza kuboresha sera na kuwa
na programu ambazo zitasaidia katika makuuzi ya watoto wa kitanzania.
Kupitia
mkutano huo wadau watapata fursa ya kuwa na uelewa wa pamoja, kushirikisha
uzoefu kati ya nchi moja na nyingine pamoja na kushawishi wadau kuweka nguvu ya
pamoja kwa ajili ya watoto.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Cha Aghakan Tanzania na Taasisi ya IHD Profesa.
Kofi Marfo amesema kuwa maendeleo na makuzi ya watoto hutegemea wazazi, familia na jamii
kwa ujumla amesisitiza pia suala la lishe bora kwa watoto, kukua na kuandaa vituo
vya afya na hospitali kwa ajili ya upatikanaji wa huduma zilizo bora.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.