Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.
William Ole Nasha amewataka watumishi wapya wa Wizara hiyo kuwa waadilifu
katika utendaji kazi pamoja na kutunza siri katika maeneo wanayofanyia kazi.
Naibu Waziri
Ole Nasha ametoa rai hiyo mjini Dodoma wakati wa akifunga mafunzo kwa waajiriwa
wapya wa Wizara hiyo, mafunzo ambayo yamelenga kuwakumbusha taratibu, sheria na
miongozo ya kazi inayotakiwa katika utumishi wa umma.
Naibu
Waziri huyo amesema anaamini mafunzo yaliyotolewa yatawawezesha kuwa watumishi
bora wa umma ambao wanafahamu vema mipaka ya kazi, taratibu za kiutumishi
lakini pia haki na wajibu katika utendaji kazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,
Mhe.William Ole Nasha akifunga mafunzo ya watumishi wapya wa Wizara hiyo ambapo
amewataka kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma,ikiwa ni pamoja na kutunza
Siri za ofisi.
Pamoja
na mambo mengine Naibu Waziri Ole Nasha amemuagiza Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali watu wa Wizara hiyo Moshi Kabengwe kuandaa utaratibu wa mafunzo
kwa watumishi wengine wa Wizara hiyo ili kuwakumbusha taratibu, kanuni na
miongozo kwa lengo la kuepuka ukiukaji wa maadili na pia kuleta chachu ya mabadiliko
katika utendaji kazi miongoni mwa watumishi.
Nae mmoja
wa watumishi aliyeshiriki mafunzo hayo Lazaro Julius kutoka Ofisi ya
Kamishna wa Elimu wa Wizara hiyo amesema mafunzo hayo ni muongozo thabiti
katika kutekeleza majukumu ya kazi za kila siku katika utumishi wa umma ambapo
ameahidi kuzingatia na kutekeleza yote yaliyoelekezwa.
Mafunzo kwa waajiriwa wapya wa Wizara
hiyo yamefanyika kwa siku Nne kuanzia Machi 6, na yameshirikisha
waajiriwa wapya kutoka wizara ya Elimu Makao Makuu na Taasisi zilizo chini ya
Wizara hiyo.
Watumishi wapya
wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakifuatilia mafunzo Maalumu ya namna
wanavyotakiwa kutekeleza majukumu yao katika Utumishi wa Umma ambayo
yamefanyika mkoani Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.