Ole
Nasha apiga marufuku Wanafunzi wa Shule
kunyimwa vyeti kwa kutokamilisha michango
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
William Ole Nasha amepiga Marufuku Wanafunzi kunyimwa vyeti pindi wanapomaliza
shule kwa madai ya kutokamilisha michango pindi walipokuwa wanasoma.
Naibu
Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Tabora alipokutana na Wakuu wa Shule za
Msingi na Sekondari kuzungumzia namna ambavyo wanapaswa kutekeleza agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John PombeMagufuli la kukataza michango
shuleni kwa kuwa Serikali inagharamia ElimuMsingi.
Naibu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa William Ole Nasha akikagua Vifaa
vyama Maabara katika Chuo cha UalimuTabora kilichopo Manispaa ya Tabora Mkoani
humo.
Naibu Waziri huyo amesema Magufuli hajakataza
uchangiaji wahiari isipokuwa amekataza michango holela ambayo ilikuwa ikichangishwa
bila utaratibu na kumzuia Mwanafunzi kuendelea na masomo kwa madai kuwa hajachanga
mchango wa aina fulani.
‘Waraka
wa Elimu Namba 6 wa mwaka 2016 unaeleza wazi namna Elimu bila malipo itakavyotekelezwa
na nijukumu la mzazi kwa mtoto wake hivyo ni marufuku Mwanafunzi kubakizwa nyumbani
au kutopewa cheti chake anapomaliza Shule kwa madai kuwa hajakamilisha mchango fulani’.amesema
Ole Nasha
Pia ametoa rai kwa walimu wote nchini kujielekeza
kwenye jukumu lao la msingi la kufundisha badala ya kujihusisha na uchangishaji
wa mchango wa aina yoyote na kwamba michango yote ya hiari itaratibiwa na Ofisi
ya Mkurugenzi wa Halmashauri husika kupitia watendaji wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.